Tuesday, June 21, 2011

HONGERA BEST, UNASTAHILI... MMH!!

Conguratulation Elizabeth Mushi a.k.a Asha Ngedereeeeee, Hureeeeeeeee!!



DADA ZANGU WA KIBONGO ANGALIENI!

Angalieni mtoto alivyoumbika! Sasa dada zangu hapa kuna haja ya mkorogo?? Enh?? Hebu angalieni wenyewe? Jivunie ulichonacho acha kujiharibu, amakweli M/ MUNGU anaumba!

MAMBO YA BAIKOKO HAYO, UNAVYOSUSIWA SASA!!

WAREMBO WETU HAWA HAPA, AZI KWENU SASA!

Washiriki wa shindano la Urembo katika kitongoji cha Sinza wakitambulishwa mbele ya waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, kabla ya mchuano mkali utakaofanyika Ijumaa wiki hii Vatican Sinza.

WANAOTUWAKILISHA SHIDA ZETU WANAPOKUWA MAKINI KUTETEA MASILAHI YETU!

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira, akitafakari wakati wabunge wakichangia hotuba ya Bajeti ya mwaka wa fedha 2011/2012, Bungeni mjini Dodoma jana. Kutokana na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutohudhuria kikao cha Bunge juzi na jana asubuhi, Waziri Wasira ndio alikuwa akikaimu nafasi ya kiongozi wa shughuri za Serikali Bungeni.



HUYU NDIYE SHEMEJI YENU

Anaitwa Monica Petro, hapa alikuwa Hispania alikwenda kwa mafunzo ya kikazi na Ng moja hivi
Unajua tena wenzetu kabla ya mambo yote mnabadilishana mawazo na maidea
Michezo vilevile kulainisha na kuchangamsha mwili
Ikinoga inapendeza??!!
Hapa baada ya yote hayo mnakunywa chai, then mnaingia katika vikao vyenu

Hapa ilikuwa Uholanzi, kabla ya kuingia Hispania, walibadili ndege hapa.

ANGALIA HAWA NAO!

Mwanafunzi wa Kituo cha Mafunzo na Uzalishaji wa Bidhaa za Ngozi cha Kizota mjini Dodoma, Shabani Rashidi akionyesha jinsi ya kutengeneza viatu, wakati wa uzinduzi wa kituo hicho iliyofanyika mwishoni mwa wiki.

KWELI KILA MTU NA KIWANJA CHAKE! HEBU ANGALIA WANAUME WANVYOSHESHA!

Wachuuzi bidhaa mbalimbali kwenye Kituo Kikuu cha Mabasi Msamvu, Mkoa wa Morogoro, wakionyesha kwa wasafiri bidhaa hizo kama walivyokutwa jana.

MAMBO YA DODOMA

Mbunge wa Jimbo la Vunjo kupitia Tanzania Labour Party (TLP), Augustino Mrema akisindikizwa na mke wake Rose kuelekea katika ukumbi wa Bunge kuhudhuria kikao cha tisa cha Bunge mjini Dodoma jana.

AJALI HII IMETOKEA JANA MAENEO YA SUKITA, KARIBU NA TABATA MATUMBI


Wakazi wa Tabata Matumbi jijini Dar es Salaam na wapita njia wakitazama lori ililitumbukia katika daraja la Mto Msimbazi eneo hilo baada ya kuacha njia jana asubuhi.

AKINAMAMA WANAWEZA


Kinamama kikundi cha Intenational Child Support Group wa mkoani Shinyanga, kutoka kushoto, Nkwaya Stephano, Maria Charles na Mariam Datu, wakiunganisha vifaa vya umemejua jijini Dar es Salaam jana, wakati wa Kongamano la Umoja wa Mtaifa na afrika la Utumishi wa Umma.

Pande za mbali




Baada ya siku mbili wakabadilisha mandhali, si unajua Wazungu hawawezi kukaa sehemu moja