Mgonjwa anayesumbiliwa na matatizo ya moyo kwa zaidi ya miaka 11 , Sesilia Edward (katikati) akisindikizwa na Muuguzi wa Hospitali ya Regency, Mary Gomes (kushoto) na Dk Christopher Lucas, muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda india kwa matibabu.
Tuesday, September 27, 2011
Lazima kieleweke!
Igunga bado, hebu tuombe mambo yaende vizuri Inshaallah
Ajali haina kinga, IGP chupu chupu
Malori saba ya sukari yakamatwa Tarime
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Deusdedit Kato (kushoto), akiwa na maofisa wa jeshi hilo mbele ya magari yaliyokamatwa kwa madai ya kukutwa yamebeba sukari kupeleka kuuzwa nchini Kenya.
Polisi Mkoa wa Tarime/ Rorya wamekamata malori saba ya sukari yaliyobeba tani 93.70, kutokana na operesheni ya kupambana na magendo iliyoshamiri ya uvushaji sukari kwenda Kenya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Deusdedit Kato, alisema walikamata mifuko 49 yenye ujazo wa kilo 50 kila mmoja nyumbani kwa mkazi wa Sirari. Alisema tani 2.45 zilitoka Tarime na tani 91.25 Musoma.
Kato alisema kwenye ukamataji walibaini mbinu ya kuhamisha sukari kutoka kwenye mifuko yake ya asili na kuwekwa mifuko mingine, ambayo ilikamatwa ikiwa tupu ya Kampuni ya Sukari Kilombero, huku sukari ikiwa imeondolewa.
Alisema sukari hiyo ilikuwa imejazwa upya kwenye mifuko ya South Nyanza Sugar ya Kenya na kwamba, shughuli hiyo hufanyika nchini na nje ya mpaka wa Tanzania, ili isafirishwe kwa urahisi kwenda Kenya.
Kato alisema maghala mengi yaliyopekuliwa hayakuwa na sukari, inasadikiwa yameficha bidhaa hiyo baada ya kutangazwa operesheni na kuongeza kuwa, imebainika sukari ya Tanzania huingizwa Kenya kwa ushirikiano wa wahalifu wengine kutoka Kenya.
“Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na taarifa za kiintelijensia, tumeendesha operesheni hii kwa kukagua maghala yote na kuwahoji wahusika. Pia, tumeongeza doria kwenye njia zote za panya na halali, tumekamata mifuko ya sukari mingine ni ya hapa Tarime na malori mengine yamekamatiwa Musoma wakidai kuwa walikuwa wanakuja kuuza Tarime," alisema