Mwandishi Wetu, Kampala
KIKOSI maalumu cha majeshi ya Uganda bado kinaendelea kumsaka mbabe wa kivita kiongozi wa kundi la waasi la lijulikanalo kama “Lords Resistance Army ‘ Joseph Kony.
Kikosi hicho kimedaiwa kusonga mbele katika msitu mmoja mkubwa uliopo katikati ya Afrika ikiwa ni kile walichodai kumsaka kiongozi huyo.
Kikosi hicho maalumu chenye watu 59kinachoitwa 77 ndicho kinachoongoza katika mkakati huo wa kimataifa wa kumsaka na hatimaye kumtia mbaroni Joseph Kony na wapiganaji wake waliobakia la kundi la waasi la Lords Resistance Army (LRA).
Inadaiwa kwamba Kony anaendelea kuwa mwenyeji wa misitu hiyo iliyopo katika mipaka ya Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambayo ni maficho yanayopendwa sana na LRA tangu kikundi hicho kilipokimbia kutoka Nchini Uganda.
“tutahakikisha tunawakamata watu hawa ma kuwarudisha nyumbani, ingawa ni kazi ngumu sana “alisema mmoja kati ya wanajeshi wa kikosi hicho maalumu.
Wanajeshi hao wanaimani kabisa kwamba Kony na kundi lake hilo la kihalifu bado wanaishi msituni kwa muda wote huo, huku wakiendelea kuwateka watoto na kuwatumia katika kundi hilo.
Pia wanadai kwamba chakula wanachokula ni viazi mwitu, pamoja na mifugo ambayo wamesema ni ya wizi huku wakinywa maji ya mito.