Monday, October 3, 2011

Msaada, msaada, msaada kwa ndugu yetu


Ramadhan Said, mkazi wa Kijiji cha Mtonga, wilayani Korogwe, anaomba wasamaria wema kumsaidia fedha za kugharimia matibabu ya miguu yake ambayo ina matatizo ya fangasi sugu.

Anasema tatizo hilo lilianza Desemba mwaka jana kwa vipele na mapunye yaliyokuwa yameota miguuni, likaendelea hadi sasa na hawezi tena kutembea au kusimama.

“Tatizo hili lilianza kama mapunye miguuni, lakini baadaye yakaanza kupanda mapajani na hatimaye tumboni,” alisema Said


Alisema alifanya juhudi za kwenda Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, ambako aliambiwa kuwa tatizo hilo ni fangasi na kupewa dawa ambazo hadi sasa hazijamsadia.

Aliongeza kwa hali inavyozidi kuwa mbaya, ni vizuri watu wakamsaidia fedha ili zimwezeshe kwenda Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo.

“Naomba wasamaria wema wajitolee kunisaidia fedha za kunifikisha Bombo na kuniwezesha kupata matibabu kwa kuwa mimi na familia yangu hatuna uwezo huo,” alisema Said.

Alisema kwa sasa hawezi kutembea na anakabiliwa na majukumu ya familia, kwa sababu ana mke na watoto wawili ambao wanahitaji msaada wake wa hali na mali.

Kwa yeyote atakayeguswa na tatizo hili awasiliane naye kwa simu namba 0656 825139 au awasilishe mchango wake ofisi za Mwananchi zilizopo Tabata relini, Dar es salaam


Mapaka tunakomaa nao, mpaka kieleweke

Waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakisubiri abiria kituo cha teksi kilichopo makutano ya Mtaa wa Likoma na Uhuru, Dar es Salaam. Bodaboda siku za karibuni zimekuwa na mivutano na wenye teksi kutokana na kutokuwa na vituo maalumu.

Libeneke la Sayansi, mpaka kieleweke

Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kutoka kushoto ni Roselyne Sadiq, Grace Jeremia, Raudha Mwasha na Elinaike Mtei,wakiwa wameshika Laptop walizopewa na mradi wa kuhamasisha wasichana kujiunga na masomo ya sayansi na ufundi unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Italia(IDC) juzi.

Mpira wa Bongo na wachezaji wetu, kazi kwelikweli

Huyu ni mchezaji wetu wa Kitanzania, hebu angalia mwenyewe hapa ni mbele ya halaiki. Ilikuwa ni siku Taifa Stars iliporudi nyumbani baada ya kushinda nje ya nchi

Mpaka sasa bado hakijaeleweka, hatujui nani mshindi Igunga!!

Wananchi mjini Igunga wakiwa wamehudhuria mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, hapa il;ikuwa ni siku ya mwisho kabla ya uchaguzi kufanyika.

Dar es Salaam bwana.. Mvua kidogo tabu tupu!

Mwendesha pikipiki akipita kwa taabu kwenye maji yaliyofurika katika eneo la Akiba jijini Dar es Salaam kufuati mvua zilizonyesha jana.