Friday, July 15, 2011


Lady Gaga apigwa mawe

SI siri mwanamuziki Lady Gaga ana mashabiki kibao lakini ana maadui wengi pia.
Gaga alikutana na watu wanaomchukia pale alipotua Australia na kujikuta akipigwa na mayai.
Alikutwa na mkasa huo wakati akiwasili katika klabu ya usiku ya ARQ huko Sydney, Australia.
Gaga alikuwa amezingirwa na mashabiki wake na walinzi lakini shabiki anayemchukua alirusha yai ambalo lilimpiga kichwani.
Mtu huyo anadaiwa kuchukizwa na kitendo cha Gaga kupewa uraia wa Australia na Meya wa Sydeny.

Foxy Brown kushtakiwa

FOXY Brown atapandishwa kizimbani baada ya kuvunja amri ya mahakama. Ameingia matatani baada ya kumtukana jirani yake kinyume na amri ya mahakama. Waendesha mashtaka wanadai kuwa Brown alivunja amri ya mahakama Julai 2010 baada ya kumsemea ovyo jirani yake.
Kibaya zaidi wakati akimtukana jirani huyo, Arlene Raymond, Brown aliinama na kuonyesha makalio yake na nguo ya ndani huku akiendelea kumtukana.
Watu hao wawili wamekuwa na bifu la muda mrefu. Kuna amri ya mahakama inayomzuia Brown kuzungumza na jirani huyo.

Lil Kim ajipanga upya

RAPA Lilí Kim anafanya kazi ya ziada ili kuibua kitu kipya.
Kim anataka kuhakikisha kuwa anarejea kwa kishindo katika gemu la hip hop.
Hivi karibuni alisherehekea kutimiza miaka 37, akiahidi kutoa singo mpya na albamu ya tano.
Kim amepanga kuachia wimbo wa "Looks Like Mone", ambao umetengenezwa na Rockwilder.
Mashabiki wake wanataka kuona Kim anaweka matatizo yake pembeni na kutoa nyimbo kali.

Nicki Minaj apigwa konde

RAPA Nicki Minaj alipigwa ngumi na mchumba wake Safaree baada ya kutokea ubishi katika hoteli moja huko Dallas.
Minaj alipigwa ngumi hiyo mdomoni na Safaree wakati wakiwa chumbani mwao.
Minaj, hata hivyo, amedai kuwa hana mpango wa kufungua mashtaka dhidi ya mtu huyo.
Mara ya kwanza rapa huyo hakutaka kusema alikuwa anagombana na nani ingawa ilikuja kujulikana alikuwa Safaree.
Inadaiwa ubishi wa watu hao wawili ulitokea katika bwawa la kuogelea la hoteli hiyo.
Mzozo ulizidi wakaenda kwenye chumba chao na ndipo Safaree akarusha ngumi.
Minaj aliomba wafanyakazi wa hoteli kuita polisi baada ya kutokea ugomvi huo na walifika mara moja na Safaree alikamatwa ingawa hakufunguliwa mashtaka.


Shakira, Pique wafunga baa

Mwanamuziki Shakira na mpenzi wake Gerard Pique walifunga baa baada ya kujirusha kisawasawa huko Miami, Marekani.
Shakira na Pique anayechezea Barcelona ndio walikuwa watu wa mwisho kuondoka katika klabu ya usiku ya Miami Beach.
Walikuwa na rafiki zao, ambao walifunga nao safari ya mapumziko nchini Marekani.
Watu hao wawili walionekana wamechoka wakati walipokuwa wanatoka nyakati za alfajiri kwenye ukumbi huo wa disko usiku wa kuamkia Jumatano iliyopita.
Walikuwa muda mwingi wakicheza disko na watu wengi walianza kuondoka mapema lakini wao walikaa hadi mwisho.
Shakira na Pique walitoka baadaye wakisindikizwa na walinzi na wapambe kibao.

NI uchakachuaji kwa kwenda mbele!


Gari la Mkuu wilaya ya Serengeti Mkoani Mara likifanyiwa matengenezo baada ya kuwekewa mafuta yaliyochakachuliwa kwa maji mjini Mugumu juzi. Jumla ya magari sita ya watu binafsi na serikali yalishindwa kutembea kutokana na kuwekewa mafuta hayo katika gereji moja (juna tuanalo).


Ukaguzi: Nani mwenye kitambi??


Ofisa wa Jeshi nchini Japan akikagua kikosi maalumu cha ulinzi kabla ya sherehe ya kumkaribisha Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani, Mike Mullen iliyofanyika katika uwanja wa Wizara ya Ulinzi nchini humo jana. Mullen anapewa heshima hiyo kutokana na mchango wa kijeshi aliyoutoa kwenye Jeshi la Japan.