Monday, October 24, 2011

Gaddafi mafanikio, wosia wake waanikwa



SIKU chache baada ya kuuawa kwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi, walibya na dunia kwa ujumla imeingia katika mitizamo tofauti kuhusu kiongozi huyo huku wengi wakikumbuka mafanikio aliyoleta kwa taifa hilo tofauti na viongozi wengine waliong’olewa kwa udikteta.

Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikimtangaza na kutafuta namna zote za kujenga picha ya udikteta bila kuangalia upande wa pili wa Libya iliyooachwa na Gaddafi.

Baadhi ya mambo ambayo yamekuwa yakizungumziwa ni iwapo Libya ya sasa itaweza kuneemeka na kile ambacho ilikuwa ikipata kutoka kwa kiongozi huyo, ambaye hivi karibuni aliuawa na wapinzani wake.

Gaddafi, tofauti na viongozi wengine waliowahi kutajwa kuwa madikteta duniani, ana mengi ya kukumbukwa na kusifiwa kwayo.

Baadhi ya wachambuzi wa masuala ya kisiasa na kiuongozi wamekuwa wakieleza kusikitishwa kwao na kutotambua aina ya demokrasia ambayo baadhi ya watu wa Libya wanaililia kwa sasa na iwapo itaboresha au kuharibu kabisa maisha yao.

Hii inawekwa wazi kwamba pamoja na kwamba Gaddafi ametumia fedha nyingi za Libya katika masuala binafsi, lakini je, kwa wastani Libya ni maskini? Wapo viongozi waliozitumia nchi zao na kuziharibu kabisa, Gaddafi aliwahi kuifilisi Libya?


Haya ni baadhi ya mambo ambayo Gaddafi aliyasimamia na kuyatekeleza katika utawala wake wa miaka 42 kwa Libya.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na tovuti za mawasiliano za Libya na Zimbabwe zimeeleza kuwa nchini Libya hakuna mwananchi aliyewahi kulipa bili ya umeme, umeme ulikuwa bure kwa raia wake wote.

Hakukuwa na riba katika mikopo, benki zote Libya zilikuwa chini ya Serikali, mikopo ilitolewa kwa wananchi bila riba ya kiasi chochote .

Taarifa hizo zikafafanua kuwa makazi ni haki ya msingi nchini Libya, Gaddafi aliwahi kusisitiza kwamba wazazi wake hawawezi kupata makazi hadi kila raia apate makazi. Baba wa Gaddafi alifariki dunia wakati yeye, mama yake wakiwa wanaishi katika hema.

Wanandoa wote wapya nchini humo walipata Dola 50,000 kwa Serikali kwa ajili ya kununua makazi yao kuwasaidia kuanzisha familia mpya.

Elimu na huduma za kiafya vilitolewa bure. Wakati Gaddafi nachukua nchi asilimia ya waliokuwa na elimu ilikuwa 25, kwa sasa inafikia 83.

Kwa waliotaka kuwa wakulima, walipewa ardhi bure, nyumba katika shamba lao, vifaa, mbegu na mifugo kwa ajili ya kuanzisha miradi .

Iwapo kuna waliokuwa hawawezi kupata huduma za elimu na afya wanazostahili, Serikali iliwalipia kwa ajili ya kuzipata nje ya nchi, hizi hazikuwa bure, walitakiwa kuchangia, walipata Dola2,300 kwa mwezi kwa ajili ya makazi na usafiri.

Kwa waliokuwa wakitaka kununua magari, Serikali ililipia kwa asilimia 50 ya bei. Bei ya petroli ilikuwa karibu na bure, lita ililipiwa kwa Dola 0.4.

Libya haidaiwi nje, pia ina akiba inayofikia Dola150 bilioni nje ambayo kwa sasa imezuiliwa.

Kwa waliomaliza vyuo, Serikali iliwapatia posho sawa na mshahara wa maofisa hadi watakapopata ajira yenye uhakika. Sehemu ya mauzo ya mafuta ya Libya iliwekwa moja kwa moja kwenye akaunti ya raia wake.

Kila mwanamke aliyejifungua alipata posho ya Dola5000, mikate 40 iliuzwa kwa dola0.15, asilimia 25 wa Walibya, wana shahada ya chuo kikuu.

Kama hiyo haitoshi taarifa hizo zimeeleza kuwa alisimamia mradi mkubwa kabisa wa umwagiliaji, uliopewa jina la Great Man-made River, kuhakikisha maji yanakuwepo kwenye maeneo yote ya nchi yenye jangwa.

Wakati wa vikwazo kwa Serikali yake miaka ya 1980, Libya ilikuwa miongoni mwa nchi tajiri kabisa kwa msingi wa pato la ndani, ikwa na kiwango cha juu cha maisha kuliko Japan. Ilikuwa ni nchi tajiri kuliko zote kabla ya vuguvugu la mapinduzi.

Wastani wa kiwango cha maisha kwa pato la kichwa ni Dola11,314 . Gaddafi amewahi kutumia fedha nyingi kwa ajili ya safari zake na miradi yake, lakini amefanya mabo makubwa ambayo hakuna dikteta aliyewahi kuyafanya kwa watu wake. Alirejesha pato kwa watu wake, aliwajali.

Wosia wa Gaddafi kabla ya kifo

Katika wosia wake, Kanali Gaddafi aliwaasa wafuasi wanaomuunga mkono kuendelea kupambana.

Alielezea msimamo wake kuwa amechagua kupambana hadi hatua ya mwisho na kufia katika ardhi ya Libya kuliko kuchagua njia nyepesi, ambayo kwa mtizamo wake, ni kitendo cha kujidhalilisha kisichokuwa na heshima, kukimbilia uhamishoni nje ya nchi yake, ambapo tayari alishapata ahadi nyingi za ulinzi.

Katika lugha ya Kiingereza, waraka wake wa wosia umetafsiriwa ukisomeka: “Hii ni hiyari yangu. Mimi Muammar bin Mohammad bin Abdussalam bin Humayd bin Abu Manyar bin Humayd bin Nayil al Fuhsi Gaddafi, ninaapa kwamba hakuna Mungu mwingine zaidi ya Allah na Muhammad ni Mtume wake, amani iko kwake. Ninaahidi nitakufa nikiwa Muislamu.

“Iwapo nitauawa, nitapenda kuzikwa kwa mujibu wa taratibu za kiislamu, nikiwa nimevaa mavazi nitakayokuwa nimevaa wakati kifo change kikitokea, bila mwili wangu kuoshwa, katika makaburi ya Sirte, jirani na familia na jamaa zangu.



“Nitapenda kwamba familia yangu, hasa wanawake na watoto, watunzwe vyema baada ya kifo changu. Watu wa Libya wana wajibu wa kulinda wasifu, mafanikio, historia na heshima ya waasisi na mashujaa wake.

“Watu wa Libya hawatakiwi kupuuza kujitapa na lazima wawe watu huru wa kuthaminiwa. Ninawataka wale wanaoniunga mkono kuendelea kupambana, kuwakabili wote wanaosimama kutoka nje dhidi ya Libya, leo, kesho na siku zote.

“Hata kama hatutashinda mapema, tutatoa funzo kwa vizazi vyetu vijavyo, kwamba kuchagua kulinda utaifa ni heshima na kuliuza ni uasi mkubwa ambao historia haitausahau milele, pamoja na juhudi za wengine kuwaeleza kinyume cha hayo”.

Kifo cha Gadafi Gaddafi na udhalilishaji wa maiti yake, mwanaye!


KUNA mvutano kuhusu mazishi ya marehemu Kanali Muammar Gaddafi, watu wa kabila la kiongozi huyo wa zamani wa Libya, wanadai mwili wa ndugu yao ili wauzike kwa heshima, wakati Baraza la Mpito linaweka ngumu na kusisitiza kwamba atazikwa kwa siri kubwa.

Ijumaa Wikienda, limenasa maisha ya Gaddafi saa 18 kabla ya kifo chake pamoja na danadana za mwili wa kiongozi huyo ambaye neno lake, harakati zake na fedha alizomwaga katika ufadhili, ndivyo viliwezesha kuundwa kwa Umoja wa Afrika.

Jumamosi iliyopita, Mwenyekiti wa Baraza la Mpito (NTC), Mustafa Mohammed Abdul Jalil alitarajiwa kwenda jijini Misrata kutoa tamko kuhusu mazishi hayo.

Kwa mujibu wa mtu anayedaiwa alikuwa mlinzi wa Gaddafi kabla ya kumgeuka dakika za mwisho, saa 18 kabla kiongozi huyo wa zamani wa Libya kufariki dunia, alizitumia kusali na kuweka mikakati ya kuhama Jiji la Sirte.


Wakazi wa Libya wakishuhudia mwili wa mtoto wa Gaddafi huku wakiufungua kinywa chake na kuupiga picha


Jumamosi iliyopita, Mwenyekiti wa Baraza la Mpito (NTC), Mustafa Mohammed Abdul Jalil alitarajiwa kwenda jijini Misrata kutoa tamko kuhusu mazishi hayo.

Kwa mujibu wa mtu anayedaiwa alikuwa mlinzi wa Gaddafi kabla ya kumgeuka dakika za mwisho, saa 18 kabla kiongozi huyo wa zamani wa Libya kufariki dunia, alizitumia kusali na kuweka mikakati ya kuhama Jiji la Sirte.

Mwanahabari wa Daily Mail, Andrew Malone, akishuhudia mwili wa Kanali Muammar Gaddafi.

Aliongeza kusema: “Aliwaambia wapigaji kwamba wakipata nafasi warudi kuitetea Libya na wasikubali vibaraka wa Marekani na Uingereza wafilisi mali za Walibya.”

Alisema kuwa saa tatu kabla Gaddafi na timu yake, hawajaanza kutoroka, alizungumza na wanaye kwa muda mrefu lakini akawasisitiza: “Msiumie wala msifedheheke, wakati mwingine Shetani hutumia nguvu na kufunika haki dhidi ya batili.”


Wakazi wa Libya wakishuhudia mwili wa Kanali Gaddafi na kuupiga picha


NENO LA MWISHO

Mlinzi huyo alisema, Gaddafi alijitetea kwa maneno mengi ili asiuawe lakini kauli maarufu aliitoa kwa njia ya kuuliza, “je, ninyi wanangu, mnaifahamu haki kwenye uongo?”


SAFARI YA KIFO

Alhamisi iliyopita (Oktoba 20, 2011), Gaddafi na timu yake, wakiwa kwenye magari ya kifahari, walikuwa wanahama kutoka Jiji la Sirte kuelekea mpakani. Inadaiwa walitaka kutorokea nje ya nchi, ingawa taarifa nyingine zinadai kiongozi huyo aligoma kuondoka na kusisitiza anangoja kufa kwenye ardhi aliyozaliwa.

Saa 2:30 asubuhi (saa za Libya), vikosi vya Nato na Ufaransa viliyashambulia kwa mabomu magari ya msafara wa Gaddafi. Magari 15 yaliharibiwa kwenye mashambulizi hayo, Gaddafi na timu yake walikwenda kujificha kwenye daraja la mtaro.

5:05 asubuhi, NTC ilitangaza kuwa ngome ya Gaddafi imekwisha na kilichobaki ni kutafuta masalia.

8:00 mchana, baada ya mapambano ya risasi kwisha, Gaddafi aligundulika yupo kwenye daraja la mtaro wa maji machafu amejificha.


Mwanahabari wa Daily Mail, Andrew Malone, akishuhudia mwili wa Kanali Muammar Gaddafi.


8:45 mchana mwanaume mmoja mkazi wa Sirte aliliambia Shirika la Utangazaji la Reuters kuwa alimuona Gaddafi akipigwa risasi tumboni kwa bastola yenye ukumwa wa 9mm.

8:56 mchana, Reuters ilitangaza kuwa Gaddafi alifariki dunia kutokana na majeraha baada ya mapigano ya risasi.

9:00 mchana, wapiganaji wa NTC walianza kuzunguka mitaani wanashangilia kukamatwa na kuuawa kwa Gaddafi.


10:31 alasiri, AFP ilitangaza kuwa mtoto wa Gaddafi, Muttasim amekutwa ameuawa jijini Sirte.

11:52 jioni, mwili wa Gaddafi ulifikishwa Misrata.

1:50 jioni, Aljazeera ilitangaza kuwa mtoto wa Gaddafi, Saif al Islam naye ameuawa kwenye mashambulizi hayo. Ingawa taarifa za baadaye zinasema kuwa Saif mikono yake ilikatika katika mashambulizi.

Wakazi wa Libya wakishuhudia mwili wa Kanali Gaddafi na kuupiga picha.
MAMIA ya wakazi wa Libya jana walikusanyika kushuhudia mwili wa Muammar Gaddafi mjini Misrata. Mwili wa Gaddafi ulikuwa umehifadhiwa katika chumba kimoja kilichopo eneo la biashara mjini Misrata, ambapo ulipelekwa siku ya Alhamisi alipouawa.

Maajabu ya Muammar Abu Minyar al-Gaddafi


1. There is *no electricity bill* in Libya; electricity is free for all its citizens.

2. There is *no interest on loans*, banks in Libya are state-owned and loans given to all its citizens at 0% interest by law.

3. *Home* considered a human right in Libya – Gaddafi vowed that his parents would not get a house until everyone in Libya had a home. Gaddafi’s father has died while him, his wife and his mother are still living in a tent.

4. All newlyweds in Libya receive *$60,000 Dinar* (US$50,000) by the government to buy their first apartment so to help start up the family.

5. Education and medical treatments are free in Libya. Before Gaddafi only 25% of Libyans are literate. Today the figure is 83%.

6. Should Libyans want to take up *farming* career, they would receive farming land, a farming house, equipments, seeds and livestock to kick-start their farms – all for free.

7. If Libyans cannot find the education or medical facilities they need in Libya, the government funds them to *go abroad* for it – not only free but they get US$2,300/mth accommodation and car allowance.

8. In Libyan, if a Libyan buys a *car*, the government subsidized 50% of the price.

9. The price of *petrol* in Libya is $0.14 per liter.

10. Libya has *no external debt* and its reserves amount to $150 billion – now frozen globally.

11. If a Libyan is unable to get *employment* after graduation the state would pay the average salary of the profession as if he or she is employed until employment is found.

12. A portion of Libyan *oil sale* is, credited directly to the bank accounts of all Libyan citizens.

13. A mother who *gave birth* to a child receive US$5,000

14. 40 loaves of *bread* in Libya costs $ 0.15

15. 25% of Libyans have a *university degree*

16. Gaddafi carried out the world’s largest *irrigation* project, known as the Great Man-Made River project, to make water readily available throughout the desert country.


Which other dictator has done much good to his people besides.


*P.S. If this is the dictator Gaddafi is, then give us one like him here in Bolehland


Wasifu wa Kanali Muammar Gaddafi





Alikuwa mtoto wa wafugaji wa Kibedui, mwenye maisha ya utata, lakini ambaye alitukuzwa sana, huku mataifa ya Magharibi yakimuona mtu wa hatari wakati wote.

Muammar Muhammad Gaddafi aliitawala Libya kwa zaidi ya miaka 40. Hadi mwanzoni mwa Machi 2011, alikuwa akiamini ndani ya moyo wake kwamba watu wake walikuwa wakimpenda na kwamba walikuwa tayari kumlinda hadi kufa kwa ajili yake.



Lakini wakati huo, tayari Gaddafi alikuwa ameshatumia njia za kikatili kuyazima maandamano dhidi yake, maandamano ambayo baadaye yaligeuka vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Kwa mujibu wa taarifa, watu zaidi ya 30,000 waliuawa kwenye vita hivyo. Mara nyingi sana, Gaddafi alitoa matamko makali wakati wa vita hivyo, ila linalojuilikana zaidi ni lile la kuwaita wapinzani wake kuwa ni panya.

Kwa kila hali, yaliyotokea ni mambo ambayo Gaddafi hakuyatarajia asilani. Mtoto huyu wa wafugaji wa Kibedui aliyezaliwa mwaka 1942, alikuja kuibuka kama mkombozi wa Walibya, alipompindua Mfalme Idriss hapo mwaka 1969.

Kuanzia hapo akaanza kujenga kile alichokiona mwenyewe kuwa ni mfumo wa kidemokrasia wa moja kwa moja. Alianzisha kamati za umma zilizoamua juu ya mustakabali wa umma na wa Serikali. Aliuita mfumo wake wa kisiasa na kiuchumi kuwa ni wa kisoshalisti, alioufafanua kwenye kijitabu chake cha Kijani.


Historia yake kiufupi

Alizaliwa mwaka 1942 katika eneo la Jangwa, kwenye mji wa Sirte, katika familia ya baba Mohamed Abdulsalama Abuminiar na mama Aisha Ben Niran. Alijiunga na Jeshi la Libya mwaka 1965.

Alifanya mapinduzi ya Serikali yasiyo ya umwagaji damu na kumuondoa mfalme Idris katika utawala wake mwaka 1969 na kuwa mtawala wa Libya akiwa na umri wa miaka 27.

Alikuwa maarufu kwa nguo anazopenda kuvaa na walinzi wa kike wenye kubeba silaha, kiongozi huyo wa Libya pia anadhaniwa kuwa na mbinu nzuri za kisiasa kwa kuweza kuirejesha Libya kutokana na kutengwa kidiplomasia duniani.

Baada ya miongo miwili ya kutengwa katika jamii ya kimataifa, mwaka 2003, Tripoli ilikiri kuwa walifanya shambulio la Lockerbie kwa kuiangamiza kwa mabomu ndege ya Pam Am. Umoja wa Mataifa (UN) ulikubali kuondoa vikwazo dhidi ya Libya.

Baada ya miezi kadhaa, Serikali ya Kanali Gaddafi ilisitisha mipango yake ya kuunda silaha za maangamizi na hii ikarejesha ushirikiano na nchi za Magharibi.




Gaddafi ni mtu wa kipekee katika kauli zake, mienendo yake, tabia zake na mikakati yake, kwa mujibu wa Saas Djebbar, mtaalam wa siasa za Libya.

Alipokuwa kijana alivutiwa na kiongozi mzalendo wa Misri, Gamal Abdel Nasser, alipokuwa akishiriki katika maandamano dhidi ya Israel wakati wa mtafaruku wa Suez mwaka 1956.

Alipanga njama ya kupindua utawala wa kifalme alipokuwa mwanafunzi wa kijeshi alipokuwa mafunzoni Uingereza kabla ya kurejea nyumbani Libya. Alipanga mapinduzi ya Septemba 1, 1969 akiwa katika mji wa Benghazi.

Alianza kujenga itikadi zake za kisiasa mwaka 1970 na kuziandika katika kitabu chake cha kijani kibichi.

Alikitumia kitabu chake kuanzisha mfumo wa kisiasa uliojumuisha kanuni za Kiislamu na mfumo ulio tofauti na siasa za ujamaa au ubepari.

Mwaka1977 aliasisi mfumo ujulikanao kama 'Jamahiriya' au 'Taifa la Umma' ambapo raia ndio wanaoendesha uongozi wa nchi yao kupitia 'kamati za umma'.

Mfumo huo wa Gaddafi umevuka mipaka na hauhusishi mambo ya siasa tu, bali pia mambo mengine.

Akiwa safarini ng'ambo, alikuwa akitumia makazi maalum kwenye kambi iliyojengwa na hema yake ya kifahari ya Kibeduwi akiwa amefuatana na walinzi wanawake ambao, inasemekana, huwa hawapotezi umakini kazini kama walinzi wanaume.


Hema hiyo pia ilitumiwa kuwalaki wageni wa Libya na Kanali Gaddafi huendesha mikutano na mahojiano yake humo humo akipepea usinga au tawi la mitende.

Rais wa zamani wa Marekani Ronald Reagan alimwita Gaddafi 'mad dog' yaani 'mbwa kichaa' na Marekani ililipiza kisasi dhidi ya Libya kwa madai ya kuhusika na mashambulio ya anga barani Ulaya kwa kuvamia miji ya Tripoli na Benghazi mwaka 1986.

Aliposhindwa katika jitihada zake za kuzipatanisha nchi za Uarabuni katika miaka ya 90, Kanali Gaddafi alielekeza nguvu zake barani Afrika na kupendekeza 'Muungano wa Nchi' za bara la Afrika.

Alianza kuvaa mavazi yake binafsi, sare za michezo zilizo na ngao za Bara la Afrika au picha za viongozi kutoka bara hilo.

Aliwahi kuvunja na kufuta Wizara za nchi hiyo pamoja na bajeti zao, isipokuwa Wizara chache ikiwemo ya Ulinzi, Fedha na Mambo ya Nje.



Licha ya uchumi wa Libya kutoa fursa kwa wawekezaji wa nje, mabadiliko bado yanakwenda taratibu.

Vuguvugu la mageuzi dhidi yake lilipoanza mwanzoni mwa mwaka huu, aliapa kuwafuata wanaompinga nyumba hadi nyumba, mlango kwa mlango, hatua iliyoibua hasira na kuchochea harakati za kijeshi dhidi yake.

Baada ya baadhi ya askari kutangaza kujitoa katika jeshi lake na kuanzisha uasi, aliapa kwamba atapambana hadi tone la mwisho la damu litakapomwagika. Alisisitiza kwamba kamwe hatakimbia kutoka katika ardhi ya Libya, atafia katika ardhi ya mababu zake.