Friday, August 12, 2011

Tumempoteza mmoja kati ya mashujaa waliyobakia katika nchi hii


Luteni Jenerali Silas Mayunga, M/Mungu amrehemu na afanye awe mwenye kupumzika salama... Amin
Mzee huyu alikuwa mpole, anayejali, pia ni mcheshi mkizoeana, nilibahatika kuwahi kukaa katika nyumba nyumba yake ya Mabibo. Kwakweli pamoja na udogo wangu kwake aliweza kunisikiliza na kunishauri pindi ninapokuwa na tatizo.

Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa akitoa salamu zake za mwisho
Makamu wa Rais, Mheshimiwa Ghalib Bilal akitoa salamu zake za mwisho

Mjane wa marehemu naye akimuaga mumewe

Baadhi ya viongozi waliokuwapo, wakiwa pamoja na Rais wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshiwa Jakaya Kikwete

Mmoja kati ya watoto wa marehemu akitoa heshima zake za mwisho