Tuesday, July 12, 2011


Kweli Tanzania kubwa!!


Abiria waliokuwa wakisafiri kati ya Arusha, Manyara na Singida, wakitazama greda la ilikikokota roli lililoshindwa kupanda mlima Mabangi uliopo kijiji cha Masakta Wilaya ya Hanang’, kutokana na uzito uliokithiri na kusasabisa abiria hao na magari mengine kukwama kwa zaidi ya saa mbili, kabla ya mkadarasi anayejenga barabara hiyo kulivuta kwa kutumia greda.

Kweli hawa tunaowachagua wanauchungu na sisi??!!

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Lazaro Nyalandu akifatilia wakati wabunge wakichangia mjadala wa kupitisha makadirio na matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha 2011/2012, mjini Dodoma juzi.

Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni, Samuel Sitta (katikati), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Mwita (kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Stephen Wasira wakiwandani ya ukumbi wa bunge huku viti vingi vya mawaziri vikiwa wazi wakati wabunge wakichangia mjadala wa kupitisha makadirio na matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha 2011/2012, mjini Dodoma jana.


Viti vitupu hata upinzani!


Wabunge wakiwa ndani ya ukumbi wa bunge wakati wa kuchangia mjadala wa kupitisha makadirio na matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa mwaka wa fedha 2011/2012, mjini Dodoma jana.

Abbas: Mguu wagu unanitesa


Abbas Abdalaah (31) aliapoanza kuvimba uvimbe mdogo katika mguu wake wa kulia hakujua kuwa ulikuwa ni mwanzo wa ugonjwa ambao hatimaye ungemfanya ashindwe kutembea.

Ugonjwa huo ambao mpaka sasa haujulikani, umemfanya Abbas kulala kitandni muda wote akilazimika kubebwa na watu watano kumpeleka nje kujisaidia.


Matumaini aliyokuwa nayo ya kupata tiba ya ugonjwa wake, yameanza kutoweka baada ya msamaria aliyejitokeza kumpeleka Hospitali ya Seliani mjini Arusha kushindwa kutimiza ahadi yake.



Abbas ambaye ni Mkazi wa Kijiji cha Kiru Ndogo, anasema vurugu za wananchi na wawekezaji wa Bonde la Kiru, Wilaya ya Babati mkoani Manyara, ndizo anaona zimesababisha mpaka sasa asipate msaada.

“Vurugu hizi zilizoaanza Machi mwaka huu , ndizo zilizosabisha leo niwe bado hapa sina msaada, kwani mmoja wa wawekezaji katika Bonde hili alikuwa ameaahidi kunisaidia kunipeleka hospitali ya Seliani," anasema kwa uchungu akiwa amelala katika kitanda chake kilichopo sebuleni kwenye nyumba ndogo ya nyasi ya Bibi yake, Zuhura Abdalah.

Akisimulia historia ya ugonjwa wake huo, anasema alianza kuvimba kiumbe kidogo katika mguu wake mwaka 2005, wakati huo akiwa mchezaji mzuri wa mpira wa miguu kijiji hapo.

Anasema hakuwa na wasiwasi kwamba huo ungekuwa ugonjwa mkubwa ambao ungemfikisha hapo alipo.


Taratibu mguu ulianza kuvimba, hali ambayo ilimfanya baba yake mzazi, mzee Abdallah Juma mwaka 2008, kumpeleka Hospitali ya Hydom, Wilaya ya Mbulu ambako baada ya kumchunguza hawakuona ugonjwa, ingawa mguu ulikuwa umevimba.

“Hydom hawakuona ugonjwa, nikawauliza mbona bado mguu umevimba kwa nini hamuoni tatizo, wakanishauri nirudi nyumbani, “ anasimulia kwa uchungu kijana huyu mchangamfu.

Ingawa madaktari katika hospitali hiyo hawakuona tatizo lolote katika mguu wa Abbas, lakini mguu mzima ulizidi kuongezeka unene, mwaka 2009 wazazi wake wakaamua kumpeleka Hospitali ya Mission ya Dareda, Wilaya ya Babati mkoani Manyara.

Huko waligundua alikuwa na matatizo katika seli za mwili hivyo wao hawakuwa na uwezo wa kumtibu na kumshauri aende Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi mjini mkoani Kilimanjaro.

Anasema mwaka uliofuatia alikwenda KCMC ambako alifanyiwa uchunguzi na matokeo yalionyesha kwamba alikuwa na matatizo ya maji kujaa katika mguu na pia alikuwa na tatizo la nyama kuongezeka katika mguu wake.

Abbas anasema baada ya kungulika tatizo hilo aliuzwa na daktari wake kama ana uwezo wa kulipia matibabu ya ugonjwa wake nje ya nchi, lakini alisema hana uwezo.

“Baada ya kueleza kuwa sina uwezo, basi huo ukawa ndio mwisho wa uwezo wao kunisaidia, nilirejea nyumbani nikiwa bado nina uwezo wa kutembea mwenyewe,” anasema.

Hata hivyo akiwa amekata tamaa ya kupata matibabu aliendelea kuishi huku akifanya shughuli zake za kila siku kwani mbali ya mguu kuendelea kuvimba , lakini hukuwa akisikia maumivu.

Machi mwaka huu ndio mwezi ambao utabaki katika kumbukumbu zake zaidi kijana huyu, kwani ndipo aliposhindwa kutembea na kuwa mtu kulala kitandani.

Tangu wakati huu kasi ya mguu kuvimba iliongezeka huku akiwa hawezi hata kusimama kwani akitaka kutoka nje ya nyumba anatakiwa kubebwa na vijana watano wenye nguvu. Mbali ya kuvimba sasa ana kidonda ambacho kinamsumbua katika mguu huo.



Sasa walahu amefikishwa hospitali kwa ajili ya huduma


Abbas Abdalaah akiwa mapokezi hospital ya Rufaa ya KCMC iliyopo Moshi mjini mkoani Kilimanjaro akishushwa kweye gari kuingia wodini kupata matibabu.

Yangaaaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!!!!!!!!!

Hayawi hayawi sasa yamekuwa. Alikuwa ni mshambuliaji Keneth Asamoah aliyeingia akitokea benchi katika dakika 15 za mwisho wa mchezo aliunganisha vizuri kwa kichwa krosi makini ya Rashid Gumbo na kuipa Yanga ubingwa wa nne wa michuano ya Kagame Castle Cup baada ya kuichapa Simba bao 1-0 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

TFF tumewaona mashbiki hao, msitupige changa hapo!

Kaseja umeiona hii!

Shamrashamra tulizianza mapemaaaaa!
Utamu wa ushindi!
Teh... Teh... Teh... Teh....!
Angalia mpanga mzee akapagawa!