Sunday, July 10, 2011
Don't chezea Yanga!
Mashabiki wa Yanga wakishangilia mara baada ya kuwafunga watani wao wa jadi Simba 1-0 na kufanikiwa kutwaa Kombe la Kagame Uwanja wa Taifa jana
Sasa Wabongo tunaanza kuamini
Wassira akiri kulala bungeni
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira, amekiri kulala bungeni wakati kikao cha bunge kikiwa kinaendelea lakini, akalilaumu our sister paper Mwananchi, for taking a photo of him in such a circumstance.
Juni 22 mwaka huu katika toleo lake namba 04013, gazeti hili lilichapisha picha ya Wasira akiwa amefumba macho na kuinamisha kichwa begani wakati anakaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni.
"Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Steven Wasira, akitafakari wakati wabunge wakichangia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2011/1012. Kutokana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutohudhuria kikao cha bunge juzi na jana (20 na 21 Juni), Wasira ndiye aliyekuwa akikaimu nafasi ya Kiongozi wa Shughuli za Serikali bungeni," ilieleza picha hiyo.
Juzi jioni Wasira wakati akifanya majumuisho ya Matumizi ya Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu alilishambulia gazeti hili kwa kumpiga picha hiyo, akisema linaandika habari za uchochezi.
Alithibitisha madai yake hayo kwa kutumia picha hiyo aliyopigwa akionekana amelala bungeni.
“Gazeti hili lina mlengo wa kigeni kila wakati linafanya mambo ya kichochezi, hawafai hawa,” alisema Wasira.
Wasira alikiri kuwa alikuwa amesinzia wakati Bunge likiwa linaendelea lakini, akasema kitendo cha gazeti hili kutoa picha yake akionekana amelala, ni uchochezi.
“Mheshimiwa Spika, mimi siku ile nilikuwa najisikia vibaya nikapitia hapo dispensary (zahanati ya Bunge) wakanipatia dawa ya mafua,”alijitetea Wasira ambaye ni mbunge wa Bunda akibainisha kuwa kwa kawaida, dawa aliyopewa ina tabia ya kusababisha usingizi.
Kwa mujibu wa Wasira Gazeti la Mwananchi lilitoa picha hiyo kwa lengo la kuchochea huku akitaja baadhi ya habari alizodai kuwa ziliwahi pia kutolewa na gazeti hili kwa lengo la uchochezi.
“Kwa mfano gazeti hili liliandika ‘Vita ya Lowassa, Serikali ya JK sasa wazi’ na nyingine ikaandika ‘Chadema yaibwaga CCM kuhusu posho,” alisema Wasira huku akinukuu vichwa vya habari hizo.
Wasira ametoa mtazamo wake huo dhidi ya gazeti hili, karibu wiki mbili tangu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Augustino Mrema kulisifu Mwananchi kuwa ni gazeti Makini, linalotoa habari za kweli na uhakika. Mrema pia aliwahi kupigwa picha na gazeti hili akiwa amelala bungeni.
Vile vile mashambulizi ya Wasira yamekuja wakati wabunge kadhaa wamekuwa wakitumia habari zilizoandikwa na gazeti hili nukuu habari za gazeti hili kujenga hoja zao bungeni, wakilieleza bunge kuwa kutokana na umakini wake, habari zinazoandikwa na Mwananchi ni za kuaminika.
Mmoja wa wabunge hao ni Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Susan Lyimo ambaye akitumia nukuu za gazeti hili aliliambia bunge kuwa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umekuwa ukijihusisha na vitendo vya kitapeli.
“Mfuko huu umekuwa na tuhuma za kuwatapeli wananchi kwa kuwapa ahadi za wongo au zisizotimizwa kwa wakati. Mathalani Julai 15 mwaka jana, zaidi ya wanachama 200 wa mfuko huo wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam walivamia ofisi ya makao makuu ya taasisi hyo yaliyopo Morocco Jijini Dar es Salaam wakilalamika kutapeliwa fedha zao za amana,” alilalamika.
Susan akionyesha kuwa taarifa hizo ni kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi la Julai 2010 pamoja na mtandao wa YouTube, alifafanua kuwa wanachama hao walikuwa wameambiwa watoe Sh18,000 kama kiingilio cha uanachama na amana ya Sh250,000 kwa ahadi ya kukopeshwa Sh1 milioni ndani ya kipindi cha wiki moja.
Mbaya zaidi alisema, wanachama hao waliongezewa vifungu vya masharti kwenye mikataba hiyo tofauti na awali hivyo kuwaweka katika wakati mgumu wa kupata mikopo waliyokusudia.
“Mheshimiwa Spika, wananchi wamefikia hatua ya kuufananisha mfuko huu wa rais na kampuni ya DEC ambayo ambayo inatuhumiwa kuendesha mchezo wa upatu kinyume cha sheria,” alisema Susan katika hutuba hiyo ya Kambi ya Upinzani wakati ambapo pia bajeti ya Mahusiano na Uratibu Ofisi ya Rais, ilikuwa imesomwa na Wasira.
Alisema PTF ilianzishwa kwa lengo l kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kwa kuwapamikopo na maarifa lakini malalamiko ya wananchi yanaashiria mfuko huo unaenda kinyume na kazi hiyo.
“Tumegundua kuwa mikopo inayotolewa na mfuko huu imekuwa na riba sawa na taasisi nyingine zinazofanya biashara ya kukopesha fedha,” alilalamika akifafanua:
“Sisi kambi ya upinzani tunahoji, je faida inayotengenezwa na mfuko huu inakwenda wapi? Mbona haionekani kwenye mapato ya serikali?”
Kibaya zaidi kwa PTF aliema
Kwa sababu hiyo, Susan alilitaka Bunge kujadili mwenendo na utendaji wa mfuk huo na kushauri njia bora ambayo itakuwa kwa maslahi yaliyokusudiwa.
Hamza anateseka, waliosababisha wanakula raha
Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH), imethibitisha kuwa maisha ya Juma Hamza (12), aliyejeruhiwa kwa risasi na polisi wa Kituo cha Chang’ombe, Wilaya ya Temeke, yapo mashakani kutokana na majeraha aliyopata kwa kupigwa risasi sehemu ya tumbo.
“Ini liliraluliwa, kifuko cha kutunzia uchafu unaotoka kwenye ini kilitobokatoboka, utumbo umetanuka na kuna tundu ndani ya kibofu chake cha mkojo,” maelezo ya kidaktari yaliyo kwenye hati ya polisi ya matibabu (PF3) yanaeleza.
Mwezeshaji wa haki jamii Mtaa wa Mgurumbasi A, Kata ya Keko, Issa Ndambwi, anayeshughulikia masuala mbalimbali ya mtoto huyo alilieleza Mwananchi kuwa, mama yake Hamza alipompeleka kliniki wiki iliyopita, alishauriwa na daktari kuwa ikiwa wanakusudia kuchukua hatua za kisheria, wafanye hivyo mapema iwezekanavyo.
Ndambwi alisema hivi sasa kinachohitajika ni msaada wa kisheria ili kesi dhidi ya waliosababisha madhara kwa mtoto huyo ifunguliwe na kufikishwa mahakamani kujibu tuhuma ili ikithibitika, haki stahiki kwa mtoto zitendeke.
Alisema wazazi wa Hamza hawana uwezo wa kumudu gharama za kuendesha kesi, hivyo anaomba yeyote mwenye uwezo na moyo wa kumsaidia mtoto huyu, kitaalamu (kisheria) au kwa fedha awasiliane na uongozi wa gazeti hili kufanikisha dhamira ya kufungua kesi haraka kama ambavyo imeshauriwa na daktari anayemtibia.
Polisi mmoja wa Kituo cha Chang’ombe anatuhumiwa kumjeruhi tumboni kwa risasi mtoto huyo usiku wa kuamkia Oktoba 24, mwaka jana. Jeshi hilo lilieleza kuwa, Hamza alijeruhiwa kwa bahati mbaya wakati askari wakikamata watuhumiwa wa unyang’anyi kwenye ukumbi wa Jumba la Dhahabu, Keko Molemo.
Hata hivyo, wakazi wa eneo la Magurumbasi A anakoishi Hamza, walipinga vikali taarifa hiyo wakisema hakuna ukumbi wenye jina hilo eneo lilipotokea tukio hilo na kwamba, waliokamatwa ni baba mzazi wa Hamza na mpangaji mwenzake, waliotolewa vyumbani mwao walimokuwa wamelala na familia zao.
Hamza alifanyiwa upasuaji mkubwa wa pili, Mei 4, 2011 na kuruhusiwa Mei 15, akitakiwa kurejeshwa hospitalini siku tatu baadaye ili atolewe nyuzi kwenye kidonda. Lakini, uongozi wa wodi aliyokuwa amelazwa ulimnyima hati ya ruhusa kwa sababu alikuwa akidaiwa Sh50,000, hadi Juni 2, mwaka huu deni lake lilipolipwa.
Malipo hayo yalipofanywa na hati za ruhusa kukabidhiwa kwa familia ya mtoto huyo, ilibainika kuwa alitakiwa kutumia aina nne za dawa ambazo mpaka wakati huo hakuwa amezitumia na kidonda kuanza kuoza kwa kutoa maji yaliyochanganyika na usaa. Taarifa ya daktari inayoeleza kuwa mtoto huyo ameharibika vibaya katika maungo yake ya ndani, inakuja huku kukiwa na malalamiko kwamba hali hiyo inachochewa na huduma zisizoridhisha ambazo amekuwa akipata mtoto huyo.
Hii kalii!
Askari magereza wanaume mkoani Morogoro kutoka katika magereza za Kingolwira,Mtego wa simba, mahabusu mkoa, Kihonda, ofisi kuu ya gereza mkoa, Mkono wa mara, Chuo cha gereza KPF na Gereza la Kingolwira wakishindana kukuna nazi katika tamasha la askari magereza lililofanyika Kingolwira manispaa ya Morogoro.
Brazil, Argentina zajiwekea mazingira magumu Copa America
Mshambuliaji wa Brazil, Neymar (kulia) akijaribu kumtoka beki wa Paraguay, Dario Veron (katikati) na kiungo Enrique Vera wakati wa mechi ya Kundi B ya michuano ya Copa Amerika iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mario Kempes mjini Cordoba, umbali wa Km 770 Kaskazini Magharibi mwa Buenos Aires. Mechi hiyo ilimalizika kwa sare 2-2.