Monday, September 26, 2011

Mercy: aliuza maji mitaani, akawa ‘housegirl’ sasa ni tajiri



Kutoka Nigeria-Mercy Johnson Ozioma- aliazimia kuonyesha kipaji chake na kuvuka mipaka kadhaa mpaka Tanzania.

Na kweli hakufanya makosa. Alicheza filamu maarufu ya ‘She is My Sister’ akiwa na Monalisa na Steven Kanumba, waigizaji wa hapa nchini.

Mwigizaji huyu ambaye anasifika kwa umahiri wa kuigiza nafasi za kulia au kunyanyaswa, amefunga ndoa na mfanyabishara Prince Okojie, Agosti 27 mwaka huu.

Mercy ambaye wengi humsifia kwa umbile lake zuri na rangi nyeusi ya Kiafrika, takwimu zinamtaja kuwa ni mmoja waigizaji wanaoilipwa zaidi Nollywood. Mafanikio haya, yanamkumbusha safari ya maisha yake; alikotoka na hilo humtoa machozi.

Alizaliwa mwaka 1981 katika Mtaa wa Satellite, jijini Lagos, akiwa ni mtoto wa nne kati ya saba. Hata hivyo, hakuweza kumaliza shule kutokana na kukosa ada.

Anakumbuka jinsi familia yake ilivyohamia katika nyumba isiyokamilika. Anazivuta kumbukumbu hizo na kuona jinsi walivyohangaika kuweka mifuko na miti juu ya paa kuukuu na kuta za nyumba wakati wa mvua.


Shuleni alikuwa akifanywa mfano na walimu kutokana na sare zake chakavu zilizochanika kila mahali.

Makali ya maisha hayakuishia hapo, aliacha shule na kwenda kuuza maji barabarani. Anaonyesha makovu miguuni aliyoyapata wakati wa kukimbizana na askari wa Jiji.

Kama haitoshi, Mercy anaeleza jinsi alivyofanya kazi za ndani, ili tu ajipatie chochote kwa familia yake.
Anasema awali hakuwa na ndoto za kuwa mwigizaji, lakini alipoitazama filamu ya ‘Sharon Stone” iliyochezwa na Genevive Nnaji, alihamasika.


Filamu yake ya kwanza, ‘Moving Train” ya mwaka 2000 ndiyo iliyofungua pazia la mafanikio. Tangu wakati huo mpaka sasa Mercy amecheza filamu zaidi ya 70.

Si hivyo tu, bali ameshinda tuzo nyingi kutokana na umahiri wake na kutalii nchi mbalimbali duniani.

Anasema: wakati mwingine anapolia katika filamu huwa anakumbuka maisha yake ya nyuma, “Nikikumbuka huwa nampa Mungu utukufu.”

Moja ya filamu maarufu na bora alizowahi kucheza ni pamoja na ‘Kill the Bride’ ‘Last Kiss’ na ‘My Heart Your Home’

Mercy hapendi kuvaa mavazi ya gharama. Anaona ni bora atumie pesa hizo kuwasaidia watoto yatima na wenye shida kuliko kununua mikoba au viatu vya gharama.


Mercy anasema siri ya mafanikio yake ni kufanya kazi kwa bidii na kumuomba Mungu ambaye amempa nguvu na kipaji.

Msanii huyu, yupo katika mikakati ya kununua nyumba ambayo ataiita ‘The House of Mercy’ kwa ajili ya watoto waishio katika mazingira magumu.

Mpaka sasa Iraq bado!

Polisi nchini Iraq na wakishirikiana na Raia wema kubeba maiti iliyozungushiwa na Shuka, iliyouawa kwa kulipukiwa na bomu,katika mji wa Karbala,jana katika ofisi za kutolewa vitambulisho na pasi za kusafiria,bomu hilo liliua watu 9.

Kweli uongozi si mchezo!!

Rais wa zamani wa Zambia, Rupiah Banda, akibubujikwa na machozi huku mke wake Thandiwe (Kulia), akimwangalia baada ya kiongozi huyo kutoa hotuba yake kwa waandishi wa habari mjini Lusaka ya kuyakubali matokeo kuwa Michael Sata ni mshindi wa uchaguzi huo. Picha na AFP.

Risasi zarindima Igunga, wabunge wawili CCM, Waitara wahojiwa polisi


HALI ya usalama katika Jimbo la Igunga inazidi kuwa tete baada ya milio ya risasi kurindima usiku wa kuamkia jana katika tukio lenye utata mkubwa, huku vyama vya Chadema na CCM vikiendelea kushutumiana.

Wakati CCM) ikidai risasi hizo zilifyatuliwa na Mratibu wa Kampeni wa Chadema, Mwita Waitara, Chadema wanadai risasi hizo zilifyatuliwa na Mbunge wa Sumbawanga mjini, Aishi Hilal wa CCM.


Tukio hilo lilitokea saa 8:00 usiku wa kuamkia jana nje ya nyumba ya kulala wageni ya Misana Lodge ambapo magari mawili aina ya Toyota Landruicer na Toyota Prado yalivunjwa vioo.

Gari hiyo ya Toyota Landcuiser linaelezwa kumilikiwa na Mbunge Hilal na Prado inadaiwa kuwa ni ya Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Ester Bulaya, ambaye CCM kinadai kuwa wafuasi wa Chadema walitaka kumteka.

Eneo lilipotokea tukio hilo ndiko ambako wafuasi wa Chadema wanalala ikiwamo kulaza magari yao yakiwamo yanayotumika katika kampeni na magari ya wabunge hao yapo katika Kituo cha Polisi Igunga kwa uchunguzi.

Naibu Kamishina wa Polisi Isaya Mngulu, ambaye ndiye Msemaji wa Polisi katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Igunga alithibitisha jana kuwapo kwa tukio hilo na kueleza kuwa silaha iliyotumika ni bastola yenye kipenyo cha milimita tisa.


“Hatujafanikiwa kuipata bastola hiyo lakini kutokana na maganda mawili ya risasi tuliyoyaokota eneo la tukio, inawezekana silaha iliyotumika ni bastola ya milimita 9,”alisema Mngulu.

Naibu Kamishina huyo alisema tayari watu zaidi ya 10 wamekwishahojiwa na polisi na kuandikisha maelezo yao wakiwamo Wabunge hao wawili, Waitara na walinzi watatu walioshuhudia tukio hilo lenye utata.

“Mpaka sasa hatuwezi kusema vioo vya magari yale vilivunjwa kwa kutumia risasi au mawe na hili ni moja kati ya mambo tunayoyachunguza, ikiwamo ni nani hasa aliyefyatua risasi zile,” alisema Mngulu.

Katika tukio hilo, kada mmoja wa CCM aliyekuwamo katika gari la Mbunge Bulaya aliyetajwa kwa jina la Ramadhan Twaha, alidai kuwa amejeruhiwa kwa risasi katika mkono wake wa kushoto na kutibiwa kisha kuruhusiwa.

Lakini Kamishina huyo wa polisi alisema kuwa, asingependa kuingia kwa undani kuhusu tukio hilo, ila polisi wameshaanza uchunguzi.

Kwa mujibu wa Kamishina huyo, polisi walipekua chumba anachoishi Waitara pamoja na cha dereva wa moja ya magari ya Chadema, lakini hawakukuta bastola yeyote ndani ya vyumba vyao.

Eneo kulipotokea tukio hilo ni umbali wa meta 20 hivi kutoka Hoteli ya Peak ambayo wamefikia viongozi wa kitaifa wa CCM.


Maelezo ya Bulaya


Akizungumza na Waandishi wa habari jana, Mbunge wa Viti Maalumu, Esther Bulaya alidai kuwa usiku huo alikuwa ametokea Baa ya Silent Inn akiwa na wabunge wenzake wawili akiwamo Aishi.

Mbunge alidai wakati anatokea katika baa hiyo kuelekea katika Hoteli ya Peak walikofikia viongozi wa CCM, waliona gari ya Chadema ikija mbele yao katika barabara ya lami kuelekea Peak na kuwamulika kwa taa kali.

“Wakawa wanakuja kwa speed (mwendo kasi), ikabidi tuwakwepe. Wakati tunakweoa tuligonga kibao. Baada ya tukio hilo ikabidi dereva wetu ageuze gari tukaanza kukimbilia barabara ya kuelekea Singida,” alidai Bulaya.

Alidai kuwa baada ya kuwakwepa, Waitara alitoa bastola na kufyatua risasi hewani kulishambulia gari lao huku vijana wengine wa Chadema waliokuwa wamepakiwa nyuma ya gari hilo, wakirusha mawe.

“Ikabidi mimi nimpigie simu Mbunge Aeshi kumweleza kuwa hawa watu wanataka kuniteka naye akawasiliana na polisi ambao walikuja kusaidia. Baada ya Waitara kuona kuna gari linawafuata wakakimbilia porini,” alidai.


Kwa mujibu wa Mbunge huyo, baada ya kuona Waitara na kundi lake wanafuatwa ndipo walipogeuza gari na kurudi hoteli waliyofikia na kuingiza gari lao ndani ya geti na wakati huohuo, polisi wakafika.

Mbunge huyo alidai kuwa Mwita alianza kumwinda yeye na Aeshi muda mrefu. Wengine aliodai kuwa walikuwa wanawindwa ni Mratibu wa Kampeni wa CCM, Mwigulu Nchemba na Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigella.

Alifafanua kuwa juzi kabla ya tukio hilo, aliwakamata vijana wa Chadema wakiwa na fomu walizoziandaa kwa lengo la kuorodhesha wapiga kura na kununua shahada jimboni humo, kitendo kilichomuudhi Waitara.

Mbunge Aeshi anena

Mbunge huyo aliwaambia waandishi wa habari kuwa muda mfupi baada ya kuachana na Bulaya, alipokea simu kutoka kwake (Bulaya) akimwarifu kuwa amevamiwa na alikuwa akielekea Singida hivyo aende kumwokoa.

“Kwa hiyo nilimwambia dereva ageuze gari tukaanza kuwafuata nyuma kuelekea Singida na nilipowakaribia nikampigia Esther nikamwambia niko nyuma yake na nimeshalifahamu hilo gari linalomfukuza,” alisema.

Alisema baada ya kulibana sana gari hilo liliingia porini naye akalifuata huko na ndipo likageuza kurudi mjini na yeye akaendelea kulifukuza na kwamba, akiwa njiani alikutana na polisi wa doria akawaarifu.

“Polisi nao wakatufuata hadi pale wanapokaa, lakini wanaonekana ni wajanja sana maana tulikuta gati (lango) likiwa wazi gari lao likaingia moja kwa moja hadi ndani na wakati huo polisi wakafika,” alidai.

Alidai kuwa wakiwa katika taharuki hiyo, ghafla gari yake ilipigwa kwa risasi kioo cha pembeni ambayo ilipita na kuvunja pia kioo cha upande wa pili na kwamba, tukio hilo lilishuhudiwa na polisi waliokuwa eneo hilo.

Tundu Lissu awageuzia kibao CCM

Mkurugenzi wa Sheria na Katiba wa Chadema, Tundu Lissu, alisema jana kuwa vijana wao ndio waliovamiwa na kundi la Vijana wa CCM wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo la Sumbawanga mjini, Aeshi.

“Lengo lao lilikuwa ni kuchoma magari yetu moto, baada ya kugundulika kuwa wameingia katika eneo la hoteli tulipokaa, vijana wetu walianza kupiga kelele na kuizunguka ile gari ya Mbunge wa Aeshi,” alisema.


Lissu aliongeza kuwa baada ya mbunge huyo kuona amezungukwa alichomoa bastola na kufyatua risasi hewani watu wakalala chini akatoroka, lakini ile gari yake ilidhibitiwa hadi polisi walipokuja.

Alifafanua kuwa polisi walilichukua gari lile na kumtafuta Mbunge huyo na kumpeleka kituoni.

Lisu alisema anashangaa badala ya polisi kumkamata mbunge huyo kwa matumizi mabaya ya silaha, walimwachia huru.

“Badala ya kumweka ndani kama walivyowaweka ndani Wabunge wetu waliotuhumiwa kumvua yule Mkuu wa Wilaya kilemba cha kichwani wakawaachilia na badala yake wanakuja kumpekua Waitara,” alisema.

Alidai kuwa mtu aliyetoa taarifa polisi kuwa Waitara ana silaha ni Mbunge Esther Bulaya aliyekuwepo pia kwenye tukio hilo la saa 8:00 usiku na kumtuhumu kwa kuwatukana polisi alipofika kituo cha polisi Igunga.

“Yule mbunge aliyefyatua risasi yupo huru bunduki yake anayo… na Rage (Ismail) aliyekuwa na bunduki juzi kwenye mkutano wa hadhara yupo huru licha ya makatazo ya tume ya uchaguzi…,”alilalamika.

Alisema jeshi la polisi linatumika kama chombo cha mabavu badala ya kutumika kama chombo cha kulinda amani na kwamba, wakiambiwa wakamate watu wa Chadema wanawakamata bila kuuliza.

Waitara azungumza

Kwa upande wake, Mwita Waitara alisema anashangazwa na hatua ya Mbunge Bulaya kumsingizia tukio kubwa kama hilo.

Aliwaambia Waandishi wa habari kuwa wakati wa tafrani hiyo yeye alikuwa amelala chumbani kwake na alishtuka usingizini kutokana na kelele alizozisikia nje.

Waitara alisema pamoja na yeye kutokuwapo kwenye gari usiku huo, anashanagzwa na hatua ya polisi kumkamata na kumshikilia kwa saa kadhaa.

Chadema wataka mgombea

CCM aenguliwe

Lissu alisema tayari Chadema kimemwandikia barua Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi kulalamikia kitendo cha Mbunge wa Tabora mjini, Ismail Aden Rage, kutembea na bastola waziwazi hadharani.

Kutokana na kitendo hicho, Chadema kimemwomba mwenyekiti wa kamati hiyo ya maadili kukiomba mgombea wa CCM, Dalaly Kafumu, aondolewe kwenye kampeni kutokana na ukiukwaji huo wa maadili.


Lissu alisema Ibara ya 2(2) ya Maadili ya Uchaguzi ya mwaka 2010 ilivyofanyiwa marekebisho Septemba 20, mwaka huu inakataza kubeba silaha yoyote inayoweza kudhuru mtu yeyote katika mikutano ya kampeni.

Alilitaka Jeshi la polisi kumkamata Rage na wabunge waliofyatua risasi na kuwaweka rumande akisema kama hilo litafanyika ataamini jeshi hilo linatenda haki kwa usawa na bila upendeleo.

Polisi kumhoji Rage

Naibu Kamishina wa polisi, Mngulu alisema polisi watamhoji Mbunge wa Tabora Mjini Aden Rage kwa kitendo chake cha kutembea na bastola hadharani.


“Tutaanza kwa kumhoji Mheshimiwa Rage kwa nini alitembeza na bastola na uchunguzi utakapokamilika tutatuma kwa wataalamu wa sheria ili wafanye ufafanuzi kwamba katika hali ile inakuwaje,” alisema.

CCM nao watoa tamko

Katibu wa NEC Fedha na Uchumi, Mwigulu Nchemba alisema jaribio la kutaka kutekwa kwa wabunge wao wawili usiku wa kuamkia jana ni mwendelezo wa matukio ya vurugu dhidi ya wana-CCM na viongozi wake.

Nchemba alisema yeye na wabunge hao wamekuwa wakiwindwa kwa muda mrefu na Chadema baada ya wao kubadilisha upepo na kuwafanya vijana wabadilike na kuamua kukiunga mkono CCM.

Katibu huyo ambaye pia ni mratibu wa kampeni za CCM jimbo la Igunga amelaani tukio hilo na matukio mengine, akiwataka polisi kuwakamata wote waliotajwa kuhusika kuwashambulia wabunge hao.


Zitto Kabwe atua Igunga

Katika hatua nyingine Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, jana aliingia katika Jimbo la Igunga kuongeza nguvu ya kampeni kwa chama chake cha Chadema na kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wanachama na wapenzi wa chama hicho.


Friday, September 23, 2011

Tanzania yetu, tangu enzi zile mpaka sasa hali ni hii!!

Gali ilikiwa limejaza mizingo pamoja na abiria kupita kiasi kutokana na shida ya usafiri Katika Kata ya Isakamaliwa walayani Igunga juzi kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa abiria hao.

Cheki baadhi ya kazi zangu



Tuesday, September 20, 2011

Mourinho kumbadili Fergie


Kocha wa Manchester United, Alex Ferguson anataka kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho achukue nafasi yake pindi atakapoacha kazi katika klabu hiyo.
Kocha huyo anaamini Mourinho ndiye atakayelinda heshima ya Old Trafford kwa kunyakua vikombe vingi iwezekanavyo.

Ferguson, ambaye amekuwa karibu na kocha huyo wa Ureno tangu mwaka 2007 aliongeza kuwa Mourinho ana uzoefu wa kutosha na anafahamu misingi ya kazi.
Mtu mmoja ambaye anawafahamu watu hao alisema; "Alex na Jose ni watu wa karibu sana. Alex atafanya kila liwezekanalo kuhakikisha kocha huyo anatua katika klabu hiyo." Jose alikuwa na matatizo akiwa Real Madrid kutokana na kukwaruzana na watu mara kwa mara lakini Alex anafahamu namna ya kuwashawishi viongozi wa juu ili wamkubali. "Kocha huyo alijiimarisha vya kutosha alipokuwa katika Ligi Kuu England na alipoondoka alishitua watu wengi."

Rita Dominic aanza kupotea


Rita Dominic amesema kwamba si kwamba amegoma kushirikishwa kwenye filamu za wasanii wengine bali amewapa vigezo na ndio maana hatokei katika kazi nyingi siku hizi.

Msanii huyo mwenye mvuto amedai kuwa si yeye tu hata mastaa wenzake wameanza kupotea makusudi ili kuongeza ubora kwenye filamu za Nollywood.
"Siyo mimi tu hata na wengine wameanza kufanya kazi kwa masharti, si kushiriki kila filamu kwavile umepewa fedha. Ubora wa filamu umeanza kuporomoka sana Nollywood, kama mtu hataki kufanya kazi yenye ubora hatanipata wala siwezi kushiriki.
"Hakuna sababu ya kuendelea kufanya mambo ndivyo sivyo, tunataka kuhamasisha watu wafanye na kuandaa kazi nzuri."

Jamani..kha! Msinifuatefuate


Uche jombo amesisitiza kuwa amefunga mjadala unaomhusisha na mwanasoka wa Nigeria, Ikechukwu Uche na wala hataki kusikia magazeti yakiendelea kumuuliza.
Imekuwa ikiripotiwa kuwa wawili hao wana uhusiano wa kimapenzi na wana mipango ya kufunga ndoa siku zijazo. Lakini ameruka vikali na kusisitiza; "Msinifuatefuate."

"Ngoja nikusaidie kwa kuwa najua kila mtu anataka kujua nini kinaendelea kwa ubaya na uzuri. Nataka uelewe kwamba sitaki kusikia wala kuzungumzia tena hilo suala, nashangaa kila mtu anafukuafukua tu kutaka kujua nini kinaendelea,"alisema.
"Siwezi kuzungumzia chochote kuhusiana na Uche na nimefunga mjadala, sipendi muendelee kuzungumzia mambo ambayo hayapo, mnapotezea watu muda waache wasome mambo ya maana."

Kama unamtaka Shilole soma hapa


Inaezekana nafasi iko wazi, ebu jaribu! Binti anayekuja juu katika tasnia ya filamu Bongo, Zuwena Mohamed 'Shilole' amesema anapenda kuolewa na mwanaume anayejishughulisha na si kijana mvivu anayetegemea mwanamke.
Msanii huyo mwenye haiba, ambaye ameshiriki katika filamu nyingi zinazofanya vema mtaani amesema; "Sipendi mwanaume anayekaa tu bila ya kufanya kazi zaidi ya kushinda maskani tu, bali nataka mwanaume mchakarikaji, anayefanya kazi kwa nguvu kwa ajili ya kuendeleza familia yetu na kujiongezea kipato zaidi, haiwezekani kuwa na mwanaume tegemezi asiye na msaada kwa familia yake."

"Maana siku hizi kuna wanaume nao wakiona mwanamke mjasiriamali tu, hawataki kazi wakitegemea wanawake zao, wanaume wa namna hiyo kwangu marufuku siwahitaji kabisa hawana nafasi," anasema Shilole.
Msanii huyu ambaye ameshiriki katika filamu ya Mafisadi wa Mapenzi, anamiliki Duka la Nguo pamoja na duka la vinywaji linaloitwa Shilole Pub maeneo ya Mwananyamala, Dar es Salaam.

Arsenal ubingwa bye bye! Tafuteni nafasi ya nne


Ni mambo ya ajabu kuona kikosi chenye nguvu cha Arsenal kikihangaika kutaka kupanda bila mafanikio! Timu hiyo imekuwa ikijaribu kunyanyuka lakini mara kadhaa imeendelea kuzama kuelekea chini ya msimamo wa Ligi Kuu England.
Timu hiyo tayari umecheza mechi tano za Ligi Kuu England lakini imedumaa katika msimamo wa Ligi. Ilianza vibaya lakini wiki iliyopita ilizinduka baada ya kupata ushindi dhidi ya Swansea, lakini ghafla wikiendi iliyopita ilipata kibano cha mabao 4-3 kutoka kwa Blackburn Rovers. Aibu si kufungwa pekee, aibu inakuja kwa kuwa wamefungwa na klabu ambayo imekuwa ikijitahidi kutokushuka daraja.
Jambo hilo linamfanya Wenger ajikute katika maswali mengi ambayo majibu yake huenda yasipatikane katika siku za karibuni. Na huu ndio ukweli wa Arsenal kwa sasa.

Mabeki wabovu
Kuruhusu mabao manne maana yake ni kwamba kuna mashaka makubwa katika nafasi ya beki. Sasa mabeki hao tayari wameruhusu mabao 14 katika mechi tano tu, hali itakuwaje siku za usoni?
Sasa washambuliaji wapya na wa zamani wanaweza kucheza kwa makini na kusaka mabao mengi iwezekanavyo lakini kama upande wa beki umepwaya, timu haiwezi kufanya mambo ya maana, watakuwa wakibahatisha kila kukicha. Mchezaji wa zamani wa Bundesliga, Per Mertesacker ndio alionekana uchochoro kabisa.

Mertesacker vilevile alihakikisha ushindi wa Blackburn baada ya kushindwa kufunga bao kwa njia ya kichwa umbali wa mita tatu tu kutoka kwa kipa.
Ni kweli matatizo hayawezi kumwelemea mtu mmoja lakini kwa kawaida roho huuma wakati unapofahamu kwamba ulikuwa na nafasi ya kuisaidia timu yako lakini hukufanya hivyo.
Na katika matukio kadhaa beki mwingine wa kati Laurent Koscielny naye amekuwa hatoi mchango mkubwa wa kuisaidia timu yake na kuna wakati huonekana kama vile anawasidia wapinzani.
Kitendo cha kujifunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Blackburn kinaonyesha kuwa mabeki wa kocha Wenger bado wana safari ndefu kuelekea kwenye mafanikio.

Wenger mtegoni
Ni kweli kocha Arsene Wenger ni mtu anayeheshimiwa katika klabu baada ya kutoa matunda katika siku za nyuma lakini kila kiti kina mwanzo na mwisho. Kama kocha huyo hatatafuta mbinu kubwa ya kufanya timu ianze kushinda itakuwa ni kazi kubwa kuendelea kutesa katika klabu hiyo.

Mashabiki walianza kumzomea Wenger baada ya kufungwa mabao 8-2 na Manchester United na huenda kichapo kutoka kwa Blackburn kikaongeza hasira si tu kwa mashabiki bali pia kwa viongozi wa ngazi ya juu.

Washambuliaji wazuri
Arsenal ilipoanza mechi dhidi ya Blackburn Rovers ilionekana kuwa ngumu na washambuliaji walionekana kuwa imara.
Gervinho na Mikel Arteta walifunga mabao yao ya kwanza katika klabu hiyo na Marouane Chamakh naye alizifumania nyavu.
Washambuliaji walionekana kuwa makini na walionana vizuri kabla ya mabeki kusambaratika. Sasa ni wakati wa washambuliaji kujidhatiti zaidi katika kutafuta mabao mengi iwezekanavyo ili mabeki wanapofanya uzembe waweze kuwabeba.

Arsenal ifikirie nafasi ya nne
Huenda Arsenal imeanza kujitoa taratibu katika kusaka ubingwa na badala yake inabidi itoke jasho kuhakikisha inashika nafasi ya nne mwishoni mwa msimu. Itakuwa ni ndoto kwa wao kuwania ubingwa kwa kuwa katika mechi tano za awali wameshinda mara moja, wametoka sare mara mbili na kufungwa mara mbili, hizo ni mechi za awali, je mechi zijazo zitakuwaje?
Huwezi kusema kuwa timu hiyo inaweza kushuka daraja kwa kuwa ni mapema sana lakini ubingwa umeanza kuyeyuka.

Walilie bahati
Vile vile wanatakiwa kuombea bahati la sivyo kila mara wataishia kupata majonzi. Ni vigumu kuelewa waliruhusu vipi mabao manne dhidi ya Blackburn lakini unaweza kusema kuwa bahati iliwatupa mkono.

Sunday, September 18, 2011

Mendes kwenye mapenzi


Kuna taarifa kuwa wakali wa filamu, Ryan Gosling na Eva Mendes ni wapenzi.
Gosling na Mendes walinaswa na paparazzi wakiwa katika mkao ulioashiria walikuwa wapenzi.
Mastaa hao kwa sasa wako katika matayarisho ya filamu ya "The Place Beyond the Pines".
Habari hiyo inathibitisha sasa habari iliyotolewa na gazeti la Us Weekly hivi karibuni.
Pia gazeti hilo lilitoa picha ya watu hao wakiwa wameshikana mikono na kukumbatiana wakati walipotembelea Disneyland mjini Anaheim, Marekani.

Milian amzingua P.Diddy


Kivazi cha mkali wa filamu na muziki, Christina Milian kiliwaacha watu hoi waliohudhuria pati iliyoandaliwa na P.Diddy.
Christina aliyeng'ara karika filamu ya ìGhost of Girlfriends Pastî, alifika katika sherehe hiyo akiwa amevaa kaptura fupi, sidiria ya bikini na viatu virefu.
P.Diddy aliandaa pati hiyo katika klabu ya Palms Casino Resort huko Las Vegas, wikiendi iliyopita.
P.Diddy ni kati ya watu waliomsifia kimwana huyo na hata kufikia kuandika kwenye mtandao wa Twitter kuwa Christina ni moto wa kuotea mbali.

Mume wa J.Lo alonga


Miezi miwili baada ya kuachana, mume wa Jennifer Lopez, ameanika kilichosababisha kuvunjika kwa ndoa hiyo.
Marc Anthony alizungumza na televisheni ya ABC News, akidai kazi ndio ziliwafanya washindwe kuishi pamoja.
Anthony alikanusha vikali kuwa alikuwa anamnyanyasa Jennifer, ambaye ni maarufu kwa jina la J.Lo.
Mume alishikilia kuwa alikuwa bado anampenda J.Lo ila masuala ya kuwa bize ndio yaliwagonganisha.
Baada ya kuvunjika kwa ndoa hiyo, watu hao waliamua kukaa kimya.
J.Lo katika siku za karibuni amekuwa bize na kipindi cha kusaka vipaji cha American Idol.

Mtoto wa Beyonce azua mjadala


Kitendo cha Beyonce kutangaza kuwa ni mja mzito, kimezua mjadala wa jinsia ya mtoto huyo katika mitandao ya mawasiliano ya Twitter na Facebook.
Wadau wameanza kujiuliza kuwa Beyonce, ambaye atazaa na mumewe Jay-Z, atapata mtoto gani wa kwanza.
Pia watu wameanza kujiuliza kuwa mwanamuziki huyo atajifungulia wapi mtoto huyo.
Mashabiki wa watu hao wanajadili pia kama mtoto huyo ataingia katika masuala ya muziki.
Mtoto anatokana na mwanamuziki, Beyonce, ambaye ni mkali wa R&B wakati Jay Z ni rapa mahiri.

Kobe Bryant ajifananisha na nyoka





Kobe Bean Bryant ni nyota wa mpira wa kikapu, ambaye anachezea Los Angeles inayoshiriki Ligi ya Marekani (NBA).
Bryant, ambaye amezaliwa Agosti 23, 1978), ndio mfungaji mahiri wa timu hiyo.
Anajiita mwenyewe jina utani la "Black Mamba", akijifananisha na nyoka huyo, ambaye anapatikana barani Afrika.
Nyoka huyo yupo katika nchi za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Sudan, Ethiopia, Eritrea, Somalia, Kenya, Uganda, Tanzania, Msumbiji, Swaziland, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana, Afrika Kusini na Namibia.
Kobe anajifananisha na nyoka huyo kwa kuwa naye ana shabaha kubwa ya kufunga na kasi.
Nyoka aina ya Black Mamba husifika kwa kuteleza kwa kasi na kushambulia bila ya kukosea.
Black Mamba anaaminika kuwa ndio nyoka mwenye kasi zaidi duniani kutokana na uwezo wa kukimbia kilomita 20 kwa saa.
Ukiangalia na rekodi ya Kobe utagundua hajafanya makosa kujilinganisha na nyoka huyo kwani anashikilia rekodi ya kuifungia pointi nyingi zaidi Lakers.
Pia ni mtu wa pili kufunga pointi nyingi zaidi katika mchezo mmoja wa NBA. Amewahi kufunga pointi 81. Wilt Chamberlain ndio anashikilia rekodi kwa kufunga pointi 100 katika mechi moja, aliyoweka mwaka 1962.
Kobe pia ni miongoni mwa watu watatu waliofunga pointi nyingi zaidi katika historia ya NBA.
Ana utajiri wa kiasi cha Dola 200 milioni (Sh. 18 bilioni za Kenya) ukitokana na mshahara wake na matangazo mbalimbali ya biashara.
Mshahara wake wa mwaka katika timu yake ya Lakers ni kiasi cha Dola 24 milioni (Sh. 2.2 bilioni za Kenya)
Ana mkataba wa matangazo na kampuni ya kutengeza vifaa vya michezo ya Nike. Pia ana mikataba na makampuni ya Coca-Cola, McDonald, NBA Infusion Ball, Upper Deck, Ferrero SpA na Russell Corporation.
Bryant pia ana mkataba wa matangazo na Shirika la Ndege la Uturuki.
Pia anafanya matangazo ya magari ya Mercedez Benz nchini China.
Kobe pia anafanya muziki, na hivi karibuni alishirikiana na mwanamuziki wa Taiwan, Jay Chou kutengeneza wimbo wa "The Heaven and Earth Challenge".
Fedha zitakazotokana na wimbo huo zitasambazwa duniani kote kwa ajili ya kutengeneza viwanja vya mpira wa kikapu.
Bryant na mkewe Vanessa wana nyumba ya thamani ya Dola 4 milioni (Sh. 375 milioni za Kenya) huko Newport Beach, Marekani.
Pia alinunua nyumba nyingine ya thamani ya Dola 13.5 milioni (Sh. 1.2 bilioni za Kenya)iliyoko Newport pia, katika Jimbo la California. Nyumba hiyo ipo katika ufukwe wa bahari kwenye eneo hilo.

Nyumba hiyo ina vyumba sita vya kulala, mabafu 11 ya kuogea, bwawa la kuogelea na gereji yenye uwezo wa kuingiza magari matano.
Bryant pia ana nyumba nyingine katika jiji la Los Angeles.
Pia ana magari aina ya Range Rover, Ferrari F430, 360 Modena, 612 Scaglietti, Bentley Continental GT, Azure Mulliner, Cadillac Escalade na 1963 Chevrolet Impala.





Kobe pia anamiliki ndege yake, ambayo hutembea nayo sehemu mbalimbali duniani.
Alianzia mpira wa kikapu katika shule ya Lower Merion kabla ya kusajiliwa na Charlotte Hornets mwaka 1996.
Alikaa kwa muda mfupi kabla ya kuchukuliwa na Los Angeles Lakers, ambako yuko hadi sasa.
Kobe amepata tuzo nyingi za NBA, ikiwamo mchezaji bora mwaka 2003, kuchezea timu ya nyota wa michuano hiyo mara 13 na medali ya dhahabu ya Olimpiki mwaka 2008.
Ni mtoto wa kocha wa zamani wa Los Angeles Sparks, Joe "Jellybean" Bryant na mama yake anaitwa Pamela Cox Bryant.
Yeye na mkewe Vanessa wana watoto wawili wa kike.

Miss Universe:Sitakuwa bishoo


Leila Lopes, ambaye ni msichana wa kwanza wa Angola kushinda taji la Miss Universe, ameahidi kusaidia watu masikini nchi mwake.
Alidai kuwa taji hilo halitamfanya aanze kuringa na kujisikia bishoo.
Mlimbwende huyo mwenye umri wa miaka 25, alisema mara zote amekuwa na huruma na watu wenye matatizo.
ìNikiwa na taji la Miss Angola nimekuwa nikisaidia watoto wa mitaani na wale wenye ugonjwa wa Ukimwi.î
Leila alieleza mradi wake unaofuata ni kusaidia wazee, ambao wanashindwa kujikimu.
ìKwa kweli sitabadilika hata baada ya kushinda taji hili kubwa. Watu wanafikiri pengine nitaanza kujisikia. Hapana haitatokea,î aliongeza Leila, baada ya kutangazwa mshindi wa taji hilo wiki hii.

J.Lo aibua na mpenzi mpya


Baada ya kuachana na Marc Anthony, mwanamuziki Jennifer Lopez amepata mpenzi mpya.
Lopez maarufu kwa jina la J.Lo hivi karibuni, alionekana na Bradley Cooper.


"Wana uhusiano wa mapenzi," alidokeza mtu mmoja, ambaye yuko karibu na J.Lo.
Baada ya habari hiyo, paparazi walifuatilia na kuwanasa katika mgawaha mmoja jijini New York.
Lopez alikuwa amevaa gauni jeupe na mara nyingi alikuwa akimkumbatia Cooper.
Lopez aliachana na Anthony hivi karibuni baada ya kuishi kwenye ndoa kwa miaka saba.

Angelina Jolie amtibulia Jennifer


Wakati Brad Pitt alipomwacha Jennifer Aniston na kumchukua Angelina Jolie, miaka sita iliyopita kulisababisha bifu huko Hollywood, Marekani.
Angelina na Jennifer mara nyingi wamekuwa wakitupiana vijembe kwenye mahojiano kuhusiana na Brad Pitt.

Jolie
Jenifer
Jennifer sasa amepata mpenzi mpya Justin Theroux na wamepanga kufunga ndoa mwakani.
Angelina, hata hivyo, amepanga kumvurugia Jennifer kwani amepanga kufunga ndoa na Brad mwakani pia.
Inasemekana Angelina anataka kumuwahi Jennifer kwa kuwa wa kwanza kufunga ndoa.
Brad inasemekana pia ameunga mkono wazo la Jennifer la kufunga ndoa.

Wes Brown achanganya soka na biashara



Wes Brown ni beki wa timu ya Sunderland inayoshiriki Ligi Kuu England, mwenye sifa ya kucheza nafasi zote za ulinzi.
Kwa muda mrefu alikuwa akichezea Manchester United lakini msimu huu amejiunga na Sunderland.
Brown ana utajiri unaokadiriwa kuwa pauni milioni 10 (Sh. 25 bilioni) ukitokana na kucheza soka na shughuli zake mbalimbali za biashara.
Ana kampuni inayoitwa Wes Brown Company, ambayo ndio inasimamia shughuli zake mbalimbali. Shughuli zake ni kama za masoko na matangazo.
Kampuni hiyo ina mali zisizohamishika zenye thamani ya pauni 598,000 (Sh. 1.5 bilioni).
Brown inasemekana anapata kiasi cha pauni 50,000 (Sh. 127 milioni) kwa wiki katika klabu yake mpya ya Sunderland.
Beki huyo anamiliki jumba lenye thamani ya pauni 4.5 milioni (Sh. 1.4 bilioni) huko Cheshire.
Jumba lenye vyumba vitano vya kulala lina chumba kikubwa kwa ajili ya kuangalia sinema, bwawa la kuogelea na studio.


Pia lina jiko la aina yake na sehemu kubwa ya uwanja, ambao kuna wakati Wes alikuwa akicheza gofu.
Wes pia ni mpenzi wa magari, na anayomiliki ni pamoja na BMW X5, Audi, Aston, Martin, Porsche, Mercedes Benz na Hummer 2.







Brown amezaliwa Oktoba 13, 1979 na alianzia soka yake katika timu ya yosso ya Manchester United mwaka 1996.
Alisajiliwa katika timu ya wakubwa mwaka 1998 na kupata nafasi katika kikosi cha kwanza katika msimu wa 1998ñ99.
Brown pia alinga'ra katika msimu wa 2000 na katika kipindi cha miaka nane ameshinda mataji mbalimbali.
Alishinda mataji ya ubingwa wa England, Kombe la FA, Kombe la Ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Brown aliitwa kwa mara ya kwanza katika kikosi cha England mwaka 1999 na alikuwemo kwenye kikosi cha Kombe la Dunia mwaka 2002.
Alicheza michuano ya awali ya Euro 2008 lakini England haikufuzu kwa fainali hizo.
Brown aliachana na timu ya England, Agosti 8, 2010, ikiwa siku moja baada ya kuitwa kwenye kikosi na kocha Fabio Capello.
Brown ameoana na Leanne Wassell, ambaye wanaishi naye Alderley Edge, Cheshire. Wana watoto wawili Halle na Lilia.

Angalia mambo haya, ukistaajabu ya...................!!!




Cheki utamu wa maziwa fresh!... Dogo mpaka kapandwa na mdadi