Thursday, October 6, 2011

Steve Jobs Earned His Place in the American Business Pantheon


Steve Jobs, who died on Wednesday, was a singular figure in American business history. He will go in the pantheon of great American entrepreneurs, inventors, and innovators, alongside John D. Rockefeller, Henry Ford, and Sam Walton.

Jobs didn't invent computer technology, or the cell phone, or the notion of digitizing music. But he invented methods, business models, and devices that turned each into significantly larger cultural and economic phenomena.


To a degree, one might look back on the arc of Jobs's career and conclude that he simply rode a series of technological waves. But Jobs, and the company he led, rode the waves while pushing back against them.

In an industry frequently hostile to design, Jobs's Apple banked on it. In an industry in which products simply got cheaper every year and everything tends toward a commodity, Apple's products were able to command a premium. And in an age of pinched consumer spending, millions of people were eager — even desperate — to shell out for the latest version of the iPod, the iPad, or the iPhone.


In an era frequently characterized by executive greed and massive pay for significant underperformance, Jobs worked for a dollar a year. At a time when many founding CEOs step down when they hit their late 40s and early 50s to chase other pursuits (a la Bill Gates), Jobs stuck with it. In an era in which many experts fretted about the ability of America's economy to thrive and innovate, Apple grew into a major exporter. Apple now represents American brands, the way McDonald's and IBM and Coca-Cola once did.


In an era in which equity values stagnated, Apple's stock thrived. The performance of the company's stock, which is now worth $322 billion, up from a few billion in 2003, is one of the great examples of value creation in modern history.

It's difficult to put a tag on what it is precisely that Jobs did. He didn't create a fundamentally new business structure, the way John D. Rockefeller did with the vertical integration of Standard Oil. He didn't democratize a product that had only been available to the very rich, as Henry Ford did with the Model T. And he didn't fundamentally alter the distribution, logistics, and production systems the way that Sam Walton did with Wal-Mart. Under Jobs, Apple simply created a bunch of really cool products that people decided they needed to have. And have again. While Apple had brilliant ads, and while Jobs was an excellent salesperson, Apple's rabid, evangelizing fans have been the most effective marketing tool. When it comes to clothes, or shoes, or cars, my kids, 13 and 9, are largely indifferent to brands. When it was time for them to get their own computer, it had to be a Mac.

There are three basic business stories: the rise, the fall, and then the comeback. Jobs provided a vivid example of each. He started Apple Computer in the 1970s out of the proverbial garage with Steve Wozniak, only to be pushed after the company had gained scale. Returning to helm the company in 1997, he led a comeback that was, in many ways, far more impressive than the original rise.



Yes, Steve Jobs got rich in the past decade. But he didn't so at the expense of his shareholders. In fact, they grew rich along with him. And Apple didn't prosper at the expense of partners. The walled-garden approach of iTunes and the Apps store goes went against the grain of the notion that everything online should be free. But it was, at root, a courageous act. And it served as a kind of affirmation for content producers. And perhaps that's why he got such good press.

Several industries in the past decade found themselves essentially powerless in the face of the internet and the advent of digital technology. But Jobs and Apple invented devices and business models that encouraged people to pay: for music, for television shows and movies, for books, and for applications. By continuing to roll out new products, Apple has really expanded the playing field for content creators. It's much more compelling to watch a movie on an iPad than it is on an iPod.


The highest form of charity is helping somebody find a job or a means to support themselves. Just so, one might argue that the highest form of business is creating a profitable enterprise that allows and encourages other people to innovate and find means to support themselves. Apple has done that time and again. Yes, the publishing and music industries have griped over payment terms. But Apple is allowing individuals and companies to reach truly massive audiences at a relatively low cost. It has rescued some markets, revived others, and created entirely new ones.

This century is only a decade old. But it's a safe bet that in 2099, when analysts and historians are looking back, Steve Jobs will be remembered as one of the giants of 21st century business.


Commeents:


Steve was among the greatest of American innovators - brave enough to think differently, bold enough to believe he could change the world, and talented enough to do it.

- President Obama



He not only gave me a lot of personal advice and encouragement, he showed all of us how innovation can change lives."

- Jerry Yang, Yahoo! co-founder




For those of us lucky enough to get to work with him, it's been an insanely great honor.

- Bill Gates, Microsoft co-founder




Steve, thank you for being a mentor and a friend. Thanks for showing that what you build can change the world. I will miss you.

- Mark Zuckerberg, Facebook founder


Steve was such an 'original,' with a thoroughly creative, imaginative mind that defined an era. Despite all he accomplished, it feels like he was just getting started.

- Bob Iger, Walt Disney CEO




Monday, October 3, 2011

Msaada, msaada, msaada kwa ndugu yetu


Ramadhan Said, mkazi wa Kijiji cha Mtonga, wilayani Korogwe, anaomba wasamaria wema kumsaidia fedha za kugharimia matibabu ya miguu yake ambayo ina matatizo ya fangasi sugu.

Anasema tatizo hilo lilianza Desemba mwaka jana kwa vipele na mapunye yaliyokuwa yameota miguuni, likaendelea hadi sasa na hawezi tena kutembea au kusimama.

“Tatizo hili lilianza kama mapunye miguuni, lakini baadaye yakaanza kupanda mapajani na hatimaye tumboni,” alisema Said


Alisema alifanya juhudi za kwenda Hospitali ya Wilaya ya Korogwe, ambako aliambiwa kuwa tatizo hilo ni fangasi na kupewa dawa ambazo hadi sasa hazijamsadia.

Aliongeza kwa hali inavyozidi kuwa mbaya, ni vizuri watu wakamsaidia fedha ili zimwezeshe kwenda Hospitali ya Mkoa wa Tanga Bombo.

“Naomba wasamaria wema wajitolee kunisaidia fedha za kunifikisha Bombo na kuniwezesha kupata matibabu kwa kuwa mimi na familia yangu hatuna uwezo huo,” alisema Said.

Alisema kwa sasa hawezi kutembea na anakabiliwa na majukumu ya familia, kwa sababu ana mke na watoto wawili ambao wanahitaji msaada wake wa hali na mali.

Kwa yeyote atakayeguswa na tatizo hili awasiliane naye kwa simu namba 0656 825139 au awasilishe mchango wake ofisi za Mwananchi zilizopo Tabata relini, Dar es salaam


Mapaka tunakomaa nao, mpaka kieleweke

Waendesha pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda, wakisubiri abiria kituo cha teksi kilichopo makutano ya Mtaa wa Likoma na Uhuru, Dar es Salaam. Bodaboda siku za karibuni zimekuwa na mivutano na wenye teksi kutokana na kutokuwa na vituo maalumu.

Libeneke la Sayansi, mpaka kieleweke

Wanafunzi wa Chuo cha Ufundi Arusha (ATC), kutoka kushoto ni Roselyne Sadiq, Grace Jeremia, Raudha Mwasha na Elinaike Mtei,wakiwa wameshika Laptop walizopewa na mradi wa kuhamasisha wasichana kujiunga na masomo ya sayansi na ufundi unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Italia(IDC) juzi.

Mpira wa Bongo na wachezaji wetu, kazi kwelikweli

Huyu ni mchezaji wetu wa Kitanzania, hebu angalia mwenyewe hapa ni mbele ya halaiki. Ilikuwa ni siku Taifa Stars iliporudi nyumbani baada ya kushinda nje ya nchi

Mpaka sasa bado hakijaeleweka, hatujui nani mshindi Igunga!!

Wananchi mjini Igunga wakiwa wamehudhuria mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo Jimbo la Igunga, hapa il;ikuwa ni siku ya mwisho kabla ya uchaguzi kufanyika.

Dar es Salaam bwana.. Mvua kidogo tabu tupu!

Mwendesha pikipiki akipita kwa taabu kwenye maji yaliyofurika katika eneo la Akiba jijini Dar es Salaam kufuati mvua zilizonyesha jana.

Sunday, October 2, 2011

Umri kikwazo cha Drogba Ulaya


Nyota wa Chelsea, Didier Drogba amewataka watu waache kuzungumza habari kuwa anataka kuondoka katika klabu hiyo kwa kuwa hafikirii kwenda popote.
Habari kwamba mchezaji huyo anataka kuhamia Ujerumani zilisambaa baada ya kuonekana akiwa katika tamasha la Oktoberfest Jumapili iliyopita huko Ujerumani.
Drogba alikwenda katika tamasha hilo akiwa na lengo la kuchangia katika mfuko wa watoto lakini waandishi wa habari walilipoti kwamba hiyo ilikuwa ni hatua ya kuelekea Bayern Munich mwakani.
"Habari hizo ni uzushi mtupu, katika umri kama wangu si rahisi kuanza maisha mapya katika klabu nyingine."

Waafrika wanaokimbizana kwa utajiri Ulaya


Waliondoka barani afrika kwenda Ulaya kutafuta utajiri wa pesa. Sasa wanashindana kuvuna fedha katika klabu mbalimbali kubwa barani Ulaya. Wafuatao ni wanasoka watano wa Afrika wanaoongoza kwa utajiri katika soka la Ulaya.

Samuel Etoo (Dola 40 milioni)

KABLA hajapata mkataba mnono akiwa na klabu ya Anzhi Makhchkahala ya Russia, Etoío ndiye baba wa fedha miongoni mwa wachezaji wa Afrika wakiwa huko ng'ambo.
Etoío anakadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 40 milioni. Kwa mwaka anaingiza kiasi cha Pauni 7 milioni. Hii ilikuwa wakati akiichezea Inter Milan kabla hajasaini mkataba mpya nchini Russia ambao unamlipa mara tatu ya kiasi hicho.
Kwa mwaka jana tu, Etoío aliingiza kiasi cha Dola 15 milioni kutokana na mikataba yake ya kibiashara na Puma na Ford pamoja na mshahara wake akiwa na Inter Milan. Kwa sasa ndiye mwanasoka anayelipwa zaidi duniani akipokea kiasi cha Pauni 365,000 kwa wiki akiwa amewaacha mbali mastaa kama Cristiano Ronaldo, Lionel Messi, Carlos Tevez, Kun Aguero na wengineo.
Aliwahi kuwanunulia wachezaji, makocha na maofisa wa timu ya taifa ya Cameroon kila mmoja saa yenye thamani ya Pauni 26,000 baada ya timu hiyo kufuzu kucheza fainali za Kombe la Dunia za mwaka jana. Etoío pia huwa hachukui pesa zozote za posho anaporudi kuichezea timu ya taifa huku akijikatia mwenyewe tiketi za ndege tofauti na wachezaji wengine.

Didier Drogba (Dola 30.7 milioni)

Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Times, Drogba ana utajiri unaokadiriwa kufikia kiasi cha Pauni 19 milioni ambazo ni sawa na Dola 30 milioni akishika nafasi ya pili nyuma ya Etoío kwa wanasoka wa Kiafrika wanaotesa Ulaya.
Kwa mshahara wa mwaka, Drogba anaingiza kiasi cha Pauni 5.5 milioni huku akiwa na mkataba unaompatia kiasi cha Pauni 105,000 kwa wiki Stamford Bridge. Drogba ana mkataba mnono na kampuni ya vinywaji baridi ya Pepsi, lakini pia ana mikataba na kampuni za Nike na Orange France.
Kudhihirisha utajiri wake, mwishoni mwa mwaka 2009, Drogba alitoa kiasi cha Pauni 3 milioni kwa ajili ya ujenzi wa hospitali katika jiji la Abidjan nchini Ivory Coast.

Michael Essien (Dola 22 milioni)


Kwa mujibu wa gazeti la Sunday Times, kiungo huyu wa kimataifa wa Ghana anakadiriwa kuwa na utajiri unaofikia Dola 22 milioni ambazo ni sawa na Pauni 14 milioni.
Misimu miwili iliyopita, Chelsea ilimuongezea mshahara wake mpaka kufikia Pauni 80,000 kwa wiki na hilo liliongeza akaunti yake kwa kiasi kikubwa kwa mujibu wa takwimu zilizofanyika Mei mwaka huu.
Dosari kubwa katika utajiri wa Essien ni kitendo kilichoripotiwa miaka ya karibuni kuwa alikuwa amemtelekeza baba yake mzazi nchini Ghana bila ya kumjali kwa kile kinachoitwa tofauti za kifamilia. Hata hivyo kwa sasa wana maelewano mazuri na amemjengea nyumba ya kuishi.

Yaya Toure (Dola 11 milioni)

Mashine hii ya Manchester City inakadiriwa kuwa na utajiri wa Dola 11 milioni ambazo kwa pesa za Kiingereza ni sawa na Pauni 7 milioni. Yaya ni mmoja kati ya wachezaji wanaolipwa fedha nyingi duniani huku mkataba wake na Man City ukimpatia kiasi cha pauni 200,000 kwa wiki.
Mapato yake kwa mwaka yanakadiriwa kufikia Pauni 8.8 milioni lakini ataingiza Pauni 4 milioni na zaidi baada ya kukatwa kodi na serikali ya Uingereza. Hata hivyo, hapa amejumlishiwa na kiasi cha fedha alizokuwa anapata akiwa na Barcelona ya Hispania.
Baada ya kuipatia Manchester City nafasi ya kucheza katika Ligi ya Mabingwa Ulaya, Toure alipata kiasi cha Pauni 800,000 kama bonasi kwa mujibu wa mkataba wake na matajiri hao wa Man City.
Pamoja na utajiri wake, Yaya hapendi maisha ya anasa na hivi karibuni aliripotiwa akiwalaumu wanasoka wengi maarufu, hasa wa Ligi Kuu England kwa kuendekeza zaidi anasa mpaka asubuhi.

Kolo Toure (Dola 11 milioni)

Kaka wa Yaya Toure ambaye kitita chake kinatoka sare na cha mdogo wake kwa sababu ghafla Yaya anavuna pesa nyingi kwa wakati mfupi wakati Kolo amevuna kwa muda mrefu tangu akiwa Arsenal.
Kolo anapokea kiasi cha Pauni 120,000 kwa wiki akiwa na Man City huku mdogo wake akipokea Pauni 200,000 kwa wiki. Kwa mwaka Kolo anaingiza kiasi cha Pauni 5.7 milioni huku akijivunia pia mkataba wake na kampuni ya Adidas.
Kolo amejikuta katika wakati mgumu baada ya kufungiwa na FA ya England kwa kufeli vipimo vya kutumia dawa za kuongeza nguvu, lakini amerudi tena uwanjani Septemba baada ya kumaliza adhabu yake ya miezi sita.

Melissa Etheridge awakawaka


MSHINDI wa tuzo za Grammy na Oscar Melissa Etheridge ambaye anasumbuliwa na kansa ya matiti alikuwa kivutio katika tamasha la Hollywood Walk of Fame lililofanyika Jumanne ya wiki hii.
Sherehe hizo zilizofanyika Hard Rock Cafe huko Hollywood zilikuwa na nia ya kuzindua kampeni ya kukusanya fedha kwa ajili ya matibabu ya wanawake wenye kansa ya matiti kote duniani na Melissa alikuwa mtu wa mfano.
Melissa mwenye umri wa miaka 50, anajulikana kutokana na nyimbo zake za 'Come to My Window' na 'I'm the Only One.'
Mwanamke huyo ambaye aligundulika kuwa na kansa ya matiti mwaka 2004, amekuwa balozi wa kampeni dhidi ya kansa kwa miaka sita.

Lil Wayne ajivunia ukubwa


Rapa na mwimbaji nyota kutoka nchini Marekani, Lil Wayne wiki hii alitimiza miaka 29 na kutangaza kuwa ni miaka yake ya mafanikio katika maisha yake na kwamba anajivunia kuwatoa wanamuziki kadhaa akiwamo Nikki Minaj.
Lil Wayne ambaye ni baba wa watoto wanne, aliandika ujumbe huo kupitia akaunti yake ya Twitter na kusisitiza kuwa ataendelea kufanya kazi ya muziki daima kwani ndio kitu alichochagua.
Rapa huyo alianza kazi ya muziki akiwa na umri wa miaka 11, wakati huo alifanya kazi na rapa B.G mwaka 1997, akiwa na umri wa miaka 15, Wayne alijiunga na B.G. Kundi hilo lilifanikiwa baadaye mwaka 1999.
Wayne ambaye kwa sasa ameshatoa albamu tisa anasifika kwa kuwa na wapenzi wengi huku akiwa na kesi mbalimbali ambazo zimewahi kumfikisha mbele ya sheria.

Jennifer Hudson kufungua gym


Mwanamuzi na mwigizaji nyota Jennifer Hudson amesema anategemea kuonyesha dhamira ya kujenga maisha yenye afya njema kwa kufungua kituo cha mazoezi maalum ya kupunguza uzito mjini Chicago.
Jennifer ambaye anatokea katika mji wa Chicago atafungua kituo hicho Jumanne ijayo ambapo ameamua kukiita Jennifer Hudson Weight Watchers Center.
Meya wa Jiji la Chicago, Rahm Emanuel anatarajiwa kuhudhuria tukio hilo litakalofanyika katika kitongoji cha Hyde Park Kusini mwa Chicago.
Walinzi wa eneo hilo wamesema kuwa katika hafla hiyo kutakuwa na mchango wa heshima kwa ajili ya watu watatu waliokufa eneo hilo.

Lady Gaga akosa mvuto


Umaarufu wa mwanamuziki Lady Gaga unaanza kuporomoka baada ya kupata mikasa mbalimbali ya maisha huku suala la kujifanya mtu wa pekee likionekana kuwakera mashabiki. Mmiliki wa televisheni Simon Cowell wiki hii amemtaja Lady Gaga kuwa mwanamuziki anayewakera watu wengi duniani.
Mchambuzi huyo wa masuala ya muziki alisema kuwa Beyonce Knowles, Katy Perry ndio wasanii wa kike wanaofanya vizuri kwa sasa na wamekuwa wakiingia katika chati ya muziki ya Billboard mara kwa mara.
"Hawa ndio wanaoonekana mara kwa mara katika vyombo vya habari kwa sasa. Lady Gaga haonekani sana kwa sababu anawakera mashabiki, labda televisheni ndio zinajitahidi kummulika," alisema Cowell.
Simon Cowell aliendelea kumponda mwanamuziki huyo kwa kusema utafiti alioufanya amegundua kuwa Gaga ni mwanamuziki anayefahamika sana kutokana na kujitangaza kupitia mavazi.

Shakira apendelewa tuzo za Latin Grammy


Waandaaji wa tuzo za Latin Grammy wamemtaja mwanamuziki mkongwe wa nchini Colombia, Shakira kuwa msanii wa mwaka baada ya jina lake kutokea katika vipengele mbalimbali vya kuwania tuzo hizo zitakazofanyika Novemba mwaka huu.
Shakira, ambaye amewahi kushinda mara tatu katika tuzo hizo atapewa tuzo ya heshima kwa sababu anakubalika katika jamii.
"Tunaona fahari kumpa heshima kubwa mwanamuziki huyu, ni mwanamke anayefanya kazi zinazowagusa wengi duniani yaani katika muziki na jamii kwa jumla," alisema Rais wa Latin Recording Academy, Gabriel Abaroa.
Shakira 34, ambaye anatambulika duniani kwa kibao cha "Hips Don't Lie" alianza kuwa maarufu kama mwanamuziki na mwimbaji mapema mwaka 1990, ambapo aliimba nyimbo za Kilatini na muziki wa Mediterania

Mourinho awafukuza kazi makocha Inter Milan


Pamoja na kwamba bado hajapata ubingwa Ligi Kuu Hispania tangu alipojiunga na Real Madrid Mei 31, 2010, Jose Mourinho bado ni mmoja wa makocha wenye vipaji vya hali ya juu duniani.
Alidhihirisha ubora wakati alipoipatia Inter Milan ubingwa wa Serie A, Coppa Italia na Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2010. Kitu cha kuchekesha ni kwamba miezi 15 tangu alipoondoka katika klabu hiyo tayari makocha watatu wameajiriwa na kutimuliwa. Kuna sababu kadhaa zilizosababisha hali hiyo, lakini sababu ya msingi ni makocha hao kushindwa kuchukua vema nafasi ya kocha Mourinho. Tayari Rafa Benitez, Leonardo na Gian Piero Gasperini wametimuliwa na juzi tu ameingia Claudio Ranieri.
Ranieri, alichukua kibarua wiki iliyopita baada ya kutimuliwa kwa Gian Piero Gasperini. Kwa kumbukumbu za haraka, mkanda kamili ulianza wakati mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich alipompa kazi kocha ambaye alianza kama mtafsiri wa Bobby Robson wakati alipoiongoza Barcelona, Huyo si mwingine ni Jose Mourinho. Kocha huyo tayari alikuwa amepata mafanikio katika kikosi cha FC Porto. Alipata Kombe la Uefa, 2003 akifuatia na ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliofuata ulimfanya awe amekusanya vikombe vyote muhimu akiwa nyumbani. Na baada ya hapo alitua England.
Baada ya mafanikio akiwa Chelsea kocha huyo alihamia Inter Milan alipata ubingwa wa Serie A, Ligi ya Mabingwa Ulaya mwaka 2010 kabla ya kuhamia Real Madrid, sasa anatafuta uwezekano wa kuimaliza Barcelona.
Jose alipendwa sana akiwa England hiyo ilitokana na ubora wake, alipata mafanikio ya kushangaza Italia na sasa anaendelea kusaka nafasi nzuri Hispania, wakati Mourinho akiwa na mafanikio hayo, Ranieri alikuwa Valencia ambapo baadaye aliacha kazi na kutua Parma, kisha Juventus na kumalizia Roma. Sasa kocha huyo anataka kufanya kazi ya Mourinho iliyowashinda makocha wengine.
Si vizuri kumtabiria haraka kocha huyo, lakini historia inaonyesha kwamba kama akishindwa kufikia mafanikio kama ya Mourinho anaweza kutimuliwa mapema. Makocha wa awali waliondokaje?

Rafael Benitez

Huyu alikuwa kocha wa kwanza kuchukua nafasi ya Jose Mourinho katika kikosi hicho. Alipewa kazi baada ya kutimuliwa Liverpool ambapo licha ya kwamba kikosi kilikosa uelekeo, timu ilikuwa na historia ya kupata ushindi siku za nyuma na iliwahi kupata ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya kocha huyo.
Kocha huyo aliendelea na nuksi alizotoka nazo Liverpool na viongozi wa ngazi za juu hawakuona ubunifu kutoka kwa kocha huyo na matokeo yake wakamtimua. Kilichomgharimu kocha huyo ni kushindwa kuendeleza pale alipoacha Mourinho. Ilikuwa ni majira ya Krismasi wakati mashabiki walipofahamu kuwa kocha mpya anatafutwa, lakini kitu kilichowashitua zaidi ni kuwa muhusika mwenyewe alikuwa ni mchezaji mkongwe wa wapinzani wao AC Milan, Leonardo.

Leonardo

Hakuwa mgeni San Siro, alifahamika zaidi kwa kuvaa jezi ya mistari ya rangi nyekundu na nyeusi siku za nyuma. Kocha huyo alianza vizuri lakini pia alijikuta ana kazi kubwa ya kufanya kabla ya kufikia mafanikio yaliyopatikana wakati wa Mourinho.
Inter ilijikuta ikiwa na wakati mgumu wa kuizuia AC Milan isipate Scudetto. Kitu kilichowachefua viongozi wa Inter Milan ni wakati Schalke 04 ilipoangusha mvua ya mabao 5-2 katika robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kuwavua ubingwa mabingwa hao watetezi. Kocha huyo ambaye awali alikuwa amesaini mkataba wa miezi 18 hakuwa na jipya na aling'olewa. Huyo naye aliondoka kwa sababu ile ile, alishindwa kuvaa vizuri viatu vya Mourinho.

Gian Piero Gasperini

Kocha mwingine alisakwa, awali uongozi ulitaka kumpa kazi Fabio Capello wa England lakini kocha huyo hakutaka na baadaye Gian Piero Gasperini akatupiwa mfupa uliomshinda fisi. Huyo naye aliingia katika historia ya Inter Milan ambapo ni kocha pekee aliyepewa kazi na kushindwa kupata ushindi katika mechi yoyote. Huyo hakuchukua muda mrefu, alitimuliwa wiki iliyopita.

Friday, September 30, 2011

Kweli Mwananchi linaongoza!!

Rais wa Zambia akisoma gazeti la Mwananchi siku moja baada ya kuapishwa, lililokuwa na kichwa cha habari Wapinzani wachukua Ikulu Zambia

Tuesday, September 27, 2011

Hatimaye mdogo wetu aenda India kwa matibabu

Mgonjwa anayesumbiliwa na matatizo ya moyo kwa zaidi ya miaka 11 , Sesilia Edward (katikati) akisindikizwa na Muuguzi wa Hospitali ya Regency, Mary Gomes (kushoto) na Dk Christopher Lucas, muda mfupi kabla ya kuondoka kwenda india kwa matibabu.

Lazima kieleweke!

Mkazi wa Manispaa ya Morogoro akiwa amebeba kiroba cha unga kichwani huku akiwa amepakiza kingine kwenye usukani wa baiskeli, eneo la Kituo cha daladala ziendazo nje ya manispaa hiyo.

Igunga bado, hebu tuombe mambo yaende vizuri Inshaallah

Waumini wa madhehebu ya dini ya Kikristo wakiwa kwenye maombi maalum ya kuombea Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Igunga unatalajiwa Jumapili hii kufanyika kwa amani na utulivu, maombi hayo yalifanyika kwenye uwanja wa Sokoine mjini Igunga juzi jioni.

Ajali haina kinga, IGP chupu chupu

Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema (kulia) akifalijiwa na msamaria mwema baada ya kunusurika katika ajali ya gari iliyotokea juzi katika Barabara ya Kivukoni Front, mbele ya Ofisi za Takwimu na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Gari ya IGP iliyokuwa ikitokea Magogoni iligongana na gari ndogo.

Malori saba ya sukari yakamatwa Tarime

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Deusdedit Kato (kushoto), akiwa na maofisa wa jeshi hilo mbele ya magari yaliyokamatwa kwa madai ya kukutwa yamebeba sukari kupeleka kuuzwa nchini Kenya.

Polisi Mkoa wa Tarime/ Rorya wamekamata malori saba ya sukari yaliyobeba tani 93.70, kutokana na operesheni ya kupambana na magendo iliyoshamiri ya uvushaji sukari kwenda Kenya.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Deusdedit Kato, alisema walikamata mifuko 49 yenye ujazo wa kilo 50 kila mmoja nyumbani kwa mkazi wa Sirari. Alisema tani 2.45 zilitoka Tarime na tani 91.25 Musoma.

Kato alisema kwenye ukamataji walibaini mbinu ya kuhamisha sukari kutoka kwenye mifuko yake ya asili na kuwekwa mifuko mingine, ambayo ilikamatwa ikiwa tupu ya Kampuni ya Sukari Kilombero, huku sukari ikiwa imeondolewa.

Alisema sukari hiyo ilikuwa imejazwa upya kwenye mifuko ya South Nyanza Sugar ya Kenya na kwamba, shughuli hiyo hufanyika nchini na nje ya mpaka wa Tanzania, ili isafirishwe kwa urahisi kwenda Kenya.

Kato alisema maghala mengi yaliyopekuliwa hayakuwa na sukari, inasadikiwa yameficha bidhaa hiyo baada ya kutangazwa operesheni na kuongeza kuwa, imebainika sukari ya Tanzania huingizwa Kenya kwa ushirikiano wa wahalifu wengine kutoka Kenya.

“Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na taarifa za kiintelijensia, tumeendesha operesheni hii kwa kukagua maghala yote na kuwahoji wahusika. Pia, tumeongeza doria kwenye njia zote za panya na halali, tumekamata mifuko ya sukari mingine ni ya hapa Tarime na malori mengine yamekamatiwa Musoma wakidai kuwa walikuwa wanakuja kuuza Tarime," alisema

Monday, September 26, 2011

Wanawake kushiriki uchaguzi Saudia


Wanaume nchini Saudi Arabia kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo wameruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi.

Mfalme wa Saudi Arabia ametoa agizo akiwaruhusu wanawake kushiriki kama wagombea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Baraza la Ushauri.

Sheria za Saudi Arabia zinawazuia wanawake wa nchi hiyo kushiriki kwenye shughuli zozote za kisiasa na pia kuwa na simu za mkononi na vilevile leseni za kuendeshea magari.

Ukiukwaji huo wa haki za wanawake huko Saudia ni mkubwa kwani wanawake wa nchi hiyo hawaruhusiwi hata kuingia kwenye maeneo mengi ya umma bila ya kuwa na mawalii au wasimamizi wao wa kiume.


UN yaanza kuijadili Palestina



Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limeanza kushauriana kuhusiana na ombi la Palestina kutaka uwanachama kamili wa umoja huo, ingawa kura kwa ajili ya ombi hilo haitarijiwi kufanyika mnamo majuma kadhaa yajayo.


Marekani imetishia kutumia kura yake ya turufu kupinga ombi hilo, ikisisitiza kuwa ni mazungumzo tu ya ana kwa ana kati ya Israel na Palestina ndiyo yatakayoweza kuzaliwa kwa taifa la wapalestina.

Pande nne zinazojihusisha na amani ya Mashariki ya kati, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi zimekuwa katika juhudi za kutaka njia ya kuyafufua mazungumzo kati Israel na Palestina.


Bill Clinton amshambulia Netanyahu


Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, amesema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ndiye aliyesababisha kukwama mwenendo wa amani ya Mashariki ya Kati.


Katika mazungumzo yake ya kidiplomasia pembezoni mwa kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Clinton amesisitiza kuwa, Netanyahu ndiye anayebeba dhima ya kukabiliwa na mkwamo mwenendo wa amani ya Mashariki ya Kati.

Madai hayo ya Bill Clinton anayatoa katika hali ambayo, daima Marekani imekuwa ikiuunga mkono utawala wa wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi wa Palestina.

Hayo yanajiri katika hali ambayo, Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amewasilisha katika Umoja wa Mataifa ombi la Wapalestina la kutaka kutambuliwa nchi yao huru katika umoja huo, ambapo Marekani imetangaza wazi kwamba, itaupinga mpango huo na kwamba, itaupigia kura ya veto.


Prof Wangari Maathai afariki dunia



Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel kutoka Kenya, Profesa Wangari Maathai (Pichani), amefariki dunia hospitalini mjini Nairobi alikokuwa akitibiwa saratani.

Profesa Maathai, aliaga dunia juzi usiku hospitalini hapo alikokuwa anapewa matibabu.


Habari zinasema, Maathai, aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2004, alikuwa muasisi wa Shirika la Mazingira nchini Kenya.

Profesa Karanja Njoroge ambaye ni Mkurugenzi wa Green Belt Movement, shirika ambalo Prof Maathai alilianzisha amethibitisha kifo hicho.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari Prof Njoroge alisema wakati wa kifo chake Wangari alikuwa na wanafamilia na marafiki.

Alisema Prof Maathai ambaye alikuwa na umri wa miaka 71, ameacha watoto watatu, wawili wakiume na mmoja wa kike.

Waasi wagundua kaburi lenye maiti 1,270 Tripoli

Ofisa wa Baraza la Mpito nchini Libya (Kulia), akiwaonyesha wapigapicha baki la sare ya gerezani ambayo imepatikana katika kaburi la pamoja la miili ya wafungwa zaidi ya 1,270 iliyogunduliwa na baraza hilo mjini Tripoli juzi. Mabaki hayo yanadhaniwa kuwa ya wafungwa waliouawa na maofisa wa usalama mwaka 1996 katika gereza la Abu Salim nchini humo.

Baraza la Mpito nchini Libya limesema kuwa, wameligundua kaburi la pamoja mjini Tripoli ambalo lina maiti 1,270.

Mabaki hayo yanadhaniwa kuwa ya wafungwa waliouawa na maofisa wa usalama mwaka wa 1996 katika gereza la Abu Salim.

Uasi dhidi ya Kanali Muammar Gaddafi ulianza kama maandamano kutaka wakili aliyewakilisha familia za wafungwa wa Abu Salim aachiliwe huru.

Uchimbuaji wa kaburi hilo la pamoja unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Msaada kwa mama


Watoto wakazi wa eneo la Nyang'andu kata ya Kivule Wilaya ya Ilala katika jiji la Dar es Salaam, wakielekea nyumbani kwao wakiwa wamebeba mboga za majani baada ya kutoka kununua.

Baada ya vuta nikuvute ya miaka 22, Troy Davis anyongwa


Licha ya shinikizo la mataifa mbalimbali kupinga hukumu ya kifo dhidi ya Troy Davis, Jimbo la Georgia nchini Marekani, limemnyonga kijana huyo na kuvuta hisia za wanaharakati wa haki za binadamu duniani kote.

Saa 5.00 usiku kwa saa za Marekani, Davis alichomwa sindano ya sumu na akafariki dakika nane baadaye. Dakika hizi za mwisho za Davis hazikuwa ngumu kwake tu, bali kwa dunia nzima iliyokuwa upande wake.

Davis alishuhudia umauti huku akishikilia msimamo wake wa kukataa kuhusika na mauaji ya Mark MacPhail yaliyotokea mwaka 1984.


Familia ya MacPhail na marafiki walikaa kwenye safu ya mbele wakiangalia. Msimamizi wa magereza alisoma amri ya kunyongwa, akimuuliza Davis kama alikuwa na chochote cha kusema, na Davis akanyanyua kichwa na kuangalia safu ya mbele na akatoa kauli kwamba alitaka kuzungumza na familia ya MacPhail.

Akasema kwamba licha ya hisia waliyonayo familia hiyo, yeye siye aliyemuua ndugu yao. Kwamba yeye binafsi hakuhusika na kilichotokea usiku ule MacPhail alipouawa, na kwamba yeye hakuwa na bastola.


Aliiambia familia hiyo kuwa anasikitishwa na kumpoteza mpendwa wao, lakini siyo yeye aliyechukua maisha ya mtoto, baba na kaka yao.

“Mimi sikumuua ndugu yenu, hili ni neno langu la mwisho kulitamka nikiwa hai, sikumuua MacPhail, naomba Mungu awasamehe wote waliotayari kuutoa uhai wangu kwa kosa ambalo sikulifanya, hamkuweza kuujua ukweli nikiwa hai naamini ipo siku Mungu atawaonyesha ukweli.

Hukumu hii ilikuwa kwanza itekelezwe mapema siku hiyo, lakini iliahirishwa wakati Mahakama Kuu ilipokuwa ikipitia rufani ya mwisho iliyowasilishwa na mawakili wa Davis.

Hata hivyo, baadaye Mahakama hiyo iliikataa rufaani hiyo.

Kwa zaidi ya mara tatu, hukumu hii ilikuwa imecheleweshwa kutokana na hoja za mawakili kwamba mashahidi saba kati ya tisa dhidi ya Davis, aidha walijikanganya au walipotosha ushahidi wao.

Msemaji wa Shirika la Kutetea Haki za Binadamu la Amnesty International, Laura Moye, amesema kwamba hukumu hii inafadhaisha sana.


"Tumepigwa na bumbuwazi. Tumefadhaishwa na tumekasirishwa sana kwamba Serikali ya Jimbo la Georgia imemnyonga Troy Davis licha ya kuwepo ushahidi wa kutosha unaotilia shaka kesi dhidi yake.

Kesi hii ya Davis ilizua umaarufu mkubwa duniani, ambapo maandamano kadhaa ya kupinga hukumu ya kifo dhidi yake yalifanyika.

Mataifa mbalimbali duniani yalituma maombi mbalimbali kuiasa Marekani isimnyonge Davis, moja kati ya mataifa makubwa yaliyotuma maombi ni Ufaransa.

Ombi la Ufaransa lilitanguliwa na maombi kama hayo kutoka kwa watu maarufu duniani, akiwamo Mkuu wa Kanisa Katoliki, Baba Mtakatifu Benedict wa XVI, rais wa zamani Marekani, Jimmy Carter na Askofu Desmond Tutu wa Afrika ya Kusini.


Troy Anthony Davis alizaliwa Oktoba 9, 1968. Alishtakiwa kwa kosa la kumuua Mark MacPhail mwaka 1989.

Siku ya tukio Macphail aliuawa wakati akijaribu kuamua ugomvi dhidi ya watu wawili ambao inasemekana mmoja wao alikuwa Davis.

Katika ugomvi huo mmoja wao alidaiwa kufyatua risasi (Baadaye ikadaiwa kuwa ni Davis ndiye aliyefanya kitendo hicho) ambayo ilichukua uhai wa marehemu MacPhail.

Avunja rekodi kwa kuwa na ulimi mrefu zaidi duniani



Kila kiungo katika mwili wa binadamu kimetengenezwa kwa kazi na ukubwa maalum, kuzidi au kupungua kwa kiungo kimoja umbo au ukubwa wake.

Lakini baadhi ya watu wamekuwa na viungo vikubwa au vidogo kupindukia, wengine hali hiyo huwasababishia matatizo na wengine huishi bila shida yeyote.

Chanel Tapper ameingia kwenye kitabu cha rekodi ya dunia (Guinness Book of World Records) baada ya kugundulika kuwa ndiye binadamu mwenye ulimi mrefu kuliko wote duniani.

Tapper (21), mwanafunzi katika Chuo Kikuu cha California, USA, ulimi wake unaweza kufunika pua yake pamoja na kuvuka kidevu.


Ulimi wa Tapper unakadiriwa kuwa na urefu wa Sentimeta 9.75 huku wataalam wa viungo vya binadamu wakiulinganisha na urefu wa simu ya mkononi aina ya iPhone.

Mrembo huyo anasema kuwa licha ya kuwa na ulimi mrefu, hana matatizo yoyote na mtu hawezi kumgundua mpaka atoe ulimi wake nje.

Anaongeza kuwa ana uwezo wa kula vitu vilivyopo kwenye makopo membamba kwa kutumia ulimi wake na hivyo kutohitaji kijiko.

"Nasikia ladha ya chakula kama kawaida, ila nafurahi sana pindi ninapokutana na watu nikitoa ulimi wangu nje watu wanashtuka, inanifurahisha sana,” anasema.

"Wasichana na wanawake wengine wanaruka na kukimbia na ikiwa nipo katika mkusanyiko wa watu wanaambizana na kuniafuata wakiniomba nitoe tena ulimi wangu nje,” anaongeza Tapper.


Anasema mara ya kwanza kugundulika kuwa ana ulimi mrefu kuliko kawaida, alikuwa na umri wa miaka minane.

"Tulikwenda kupiga picha kwa ajili ya kuhifadhi kumbukumbu nikiwa na mama, picha mojawapo tulitoa ulimi nje na ilipotolewa ndipo tulipogundua hilo," anasema.

Anasema wengi wamekuwa hawaamini wanapomuona na kuongeza kuwa hawezi kubadilisha maumbile yake kwani ndivyo alivyozaliwa na hapati shida ya aina yoyote kutokana na kiungo hicho.

Hata hivyo, urefu wa ulimi wa Tapper huenda ni urithi kutoka kwa mama yake.

“Mama yangu ana ulimi mrefu, lakini si kama mimi. Naamini nilizaliwa pasipo kuwa na ulimi mrefu hivi, lakini uliendelea kukua kwa kadri nilivyokua," anasema.


Kuhusu mahusiano, Tapper anasema hakuwahi kupata shida ya aina yoyote kwa wapenzi aliowahi kuwa nao, kwani waliona ni jambo la kawaida, anasema kwa sasa hayupo kwenye mahusiano.

Aliyekuwa akishikilia rekodi hiyo tangu mwaka 2006 ni Stephen Taylor, raia wa Italia ambaye alikuwa na ulimi wenye urefu wa sentimeta 9.5.

Mwaka 2001 mwanadada Annika Irmler raia wa Ujerumani alishikilia rekodi hiyo kwa kuwa na ulimi wenye urefu wa sentimita 7.