Monday, August 15, 2011

Jamani hata hii ni ajira kwa watoto!! Angalia hawa!





Angalia mambo hayaaaaa!

Hapa nahisi walikuwa kama wanacheza Prakatatumba??!!

Jamani hii shule ipo hukooooo Kenya
Hata hii nayo, hukohuko kwa Kibaki

Angalia vipaji mtaani kwetu!


Angalia mtu kapewa kubwa huku akimiliki mpira, watoto wabaya hawa!
Nikagundua kuwa kuna akina Drogba wa Chelsea na Valencia wa Manchester Utd
Ona Valencia anavyonyanyasa wenzake!

Sekeseke golini

Friday, August 12, 2011

Tumempoteza mmoja kati ya mashujaa waliyobakia katika nchi hii


Luteni Jenerali Silas Mayunga, M/Mungu amrehemu na afanye awe mwenye kupumzika salama... Amin
Mzee huyu alikuwa mpole, anayejali, pia ni mcheshi mkizoeana, nilibahatika kuwahi kukaa katika nyumba nyumba yake ya Mabibo. Kwakweli pamoja na udogo wangu kwake aliweza kunisikiliza na kunishauri pindi ninapokuwa na tatizo.

Rais wa Awamu ya Tatu, Mheshimiwa Benjamin Mkapa akitoa salamu zake za mwisho
Makamu wa Rais, Mheshimiwa Ghalib Bilal akitoa salamu zake za mwisho

Mjane wa marehemu naye akimuaga mumewe

Baadhi ya viongozi waliokuwapo, wakiwa pamoja na Rais wa Jahuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshiwa Jakaya Kikwete

Mmoja kati ya watoto wa marehemu akitoa heshima zake za mwisho


Thursday, August 11, 2011

Kim Kardashian looks awful & Kris Humphries might be “the prisoner groom”






Did you know there’s a magazine called “World’s Most Beautiful”? There is, and Kim Kardashian is their first cover girl. The cover is in 3D, in case you care. That’s why Kim is wearing the 3D glasses in some of the photos. But I’m more interested in the photos where you can really see her face. Now, I have long maintained that Kim’s face has gotten a massive overhaul, and that she’s full of Botox, fillers, lip injections and God knows what else. But one thing that I rarely take into account is the fake eyelashes. They give her face such a weird look, right? It’s like she’s attached gigantic tarantulas to her eyes.



By the way, we’re in full countdown mode for Kim’s wedding. It’s next week, on the 20th. Kim has invited every dumb celebrity you can imagine, but I seriously doubt all of them are going to show up. I mean, will Jennifer Lopez come to Kim’s wedding? No, right? And while Kim obsesses over every little detail, it seems like Kris Humphries has just started to realize how deep it’s gotten. Kris tweeted yesterday, “Time is moving fast.” Ya think? Oh, what will happen if he pulls a runner? He’s the dude version of Charlene Wittstock, I think. The prisoner groom.

What’s worse? Apparently, Kim refused to invite many of Kris’s relatives, and Kris has been fighting with Kim’s mom, Kris Jenner. In Touch Weekly’s insider claims that Kris Jenner is “a stage mother with a type-A personality. She controls her daughters’ lives, and already she’s trying to control Kris’ as well. She turned into the mother-in-law from hell as soon as Kris proposed.” The insider also has Kris Jenner telling Kris Humphries, “Kim isn’t becoming a Humphries. You’re becoming a Kardashian. Deal with it!” Poor Kris Humphries.


Huyu ndiye dereva anayepaswa kuwa makini barabarani, kuchunga maisha ya abiria wake!!


Sunday, July 24, 2011


Sherzinger: Hamilton hajanichumbia

Mwanamuziki Nicole Scherzinger amekanusha vikali kuwa amechumbiwa na dereva wa magari ya Formula One, Lewis Hamilton.
Sherzinger aliandika katika mtandao wa mawasiliano wa Twitter kukanusha vikali taarifa hizo zilizosambaa kwa kasi.
Nicole aliandika; "Lewis na mimi tuliamka asubuhi na kusoma taarifa kuwa tulikuwa tumevalishana pete."
Baba wa Nicole, Alfonso Valiente ndio mtu aliyechangia kuenea kwa uvumi huo.
ìWatu hawa wamechumbiana na ninampenda sana mkwe wangu Lewis Hamilton."

Charlize, Reynolds wabambwa

Paparazzi hivi karibuni waliwanasa nyota wa filamu, Charlize Theron na Ryan Reynolds wakiwasili muda mmoja katika Uwanja wa Ndege wa Los Angeles, Marekani.
Kitendo hicho kilizidi kuthibitisha kuwa Charlize na Ryan wana uhusiano wa mapenzi.
Watu hao wawili wamekuwa wakificha suala la wao kuwa na uhusiano wa mapenzi.
Charlize ameapa kutokwenda mahali popote akiwa amefuatana na Ryan.
Mkali huyo wa filamu alieleza huwa hana utaratibu kufuatana na mtu wake kila mahali anapokwenda.
Naomi awapiga jeki Red Cross

Mwanamitindo Naomi Campbell ametoa kitita cha pauni 94,000 (sh. 231 milioni) kwa ajili ya Shirika la Msalaba Mwekundu.
Campbell ametoa fedha hizo ili kusaidia watu walioathirika na kimbunga cha tsunami nchini Japan.
Naomi hivi karibuni aliandaa maonyesho ya mavazi huko Cannes, Ufaransa kwa ajili ya kuchangia fedha za kusaidia watu wa huko Japan.
"Mara nyingi tumekuwa tukiandaa maonyesho ya mavazi sehemu mbalimbali duniani ili kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali."
Mastaa wa fani mbalimbali walichangia fedha ili kusaidia watu wa Japan, ambao pia waliathirika na kulipuka kwa mitambo ya nguvu za nyuklia.

Kim Kardashian kufunga ndoa Agosti

Harusi ya mwanamitindo Kim Kardashian na nyota wa mpira wa kikapu, Kim Humphries itakuwa Agosti 20, mwaka huu.
Kardashian alisema; ìKwa kweli nimekuwa nikiota kuolewa tangu nikiwa msichana mdogo.î
Katika sehemu ya maandalizi ya harusi hiyo, Kim alifanya vikao vingi na mahojiano na televisheni jijini New York.
Sasa ametua jijini Los Angeles ili kuendelea na maandalizi ya shughuli hiyo.
Atuhumiwa kuvunja ndoa ya Lopez

J. Lo na Levy, pia alishiriki katika tamthiria ya ITV
'Don't Mess with my Angel' au Marichuy

Mwanamitindo William Levy ndio anatuhumiwa kuvunja ndoa ya Jennifer Lopez.
Mwanamuziki Lopez, ambaye ni maarufu kwa jina la J.Lo alitangaza kutengana na mumewe Marc Anthony wiki iliyopita.

Enzi za ndoa yake na Mack Anthony

Kuna taarifa kuwa J.Lo alikuwa na uhusiano wa mapenzi wa siri na Levy.
Mwanamitindo huyo alishiriki katika video ya wimbo wa J.Lo wa ìIím Into Youî.
Levy, ambaye aliachana na mkewe mwezi mmoja baada ya kurekodi video, amekanusha vikali taarifa hizo. hiyo


"Ninachoweza kusema Jennifer si mpenzi wangu bali uhusiano wetu ni wa kikazi zaidi."


Abramovich akodisha boti lake

Mmiliki wa Chelsea, Roman Abramovich (pichani juu), anakodisha boti yake kwa bei ya kutisha ya pauni 1.25 milioni (sh. 178 milioni za Kenya)kwa wiki.
Abramovich alinunua boti kwa kiasi cha pauni milioni 750 milioni (sh. 107 bilioni za Kenya) ili kulipia boti hiyo inayoitwa Eclipse.
Boti hiyo ni ya aina yake kwani ina vifaa ya kurusha makombora ya kivita chini yake.
Gharama ya kukodisha kwa siku ni kiasi cha pauni 175,000 (sh. 25 milioni za Kenya). Gharama hizo zinajumuisha posho za wafanyakazi 70, kutumia helikopta mbili, bwawa la kuogelea, gym na saluni.
Boti hiyo ina vyumba 15 vinavyoweza kuingiza wageni 30, mabafu ya kisasa na televisheni za kisasa.

Gharama ya kuhudumia boti hiyo ni kiasi cha pauni 50 milioni (sh. 7.1 bilioni za Kenya) kwa mwaka. Gharama ya mafuta ni pauni 400,000 (sh. 57 milioni za Kenya)



Demu mwingine amwanika Cole

Mwanamke mwingine ameibuka kufichua kuwa alilala na Ashley Cole wakati akijaribu kumrudia mkewe wa zamani, Cheryl.
Collette McBarron, ambaye ni mwanamitindo alisema alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na beki huyo wa Chelsea na England.
Kitendo hicho kitazidi kumchafua Cheryl, ambaye katika siku za karibuni amekuwa akisaka suluhu na mumewe Cole.

Huyu ndiye mtuhumiwa mwenyewe, Ashley Cole
Collette, ambaye aliwahi kuwania taji la Mrembo wa Ireland: "Kwa kweli ninaposikia habari ya Cole kujirekebisha nabaki nashangaa."
Mrembo huyo, ambaye alikuwa jeshini, alisema ana picha za kuthibitisha uhusiano wao na Cole.
Mhudumu wa kwenye ndege, Kerry Meades alikaririwa na gazeti la Sunday Mirror la Uingereza wikiendi iliyopita akidai pia alikuwa anatembea na Ashley wakati akisaka suluhu na mkewe Cheryl, ambaye waliachana.


Fally Ipupa avuruga mambo Mombasa


MWANAMUZIKI maarufu kutoka Congo, Fally Ipupa alisababisha vurugu katika ukumbi wa Mamba Disco aliposusia kuhudhuria tamasha hilo lililongojewa na wakazi wengi wa mjini Mombasa kwa hamu na ghamu.
Inadaiwa kuwa Fally Ipupa alisusuia shoo hiyo kwa kuwa hakupewa malipo yake kwa wakati unaofaa.
Ni mara ya pili kwa msanii huyu kususia shoo mjini Mombasa, zote zikiwa zimeandaliwa na promota Jules Nsana wa Nsana Promotions.
Muda mfupi kabla ya saa tisa za alfajiri, Fally Ipupa aliandika kwenye Facebook kuwa: "For Organisational reasons, the organisers cancel the show in Mombasa."
Mashabiki walianza kumshambulia DJ Collo na kuharibu vifaa vyake kwa hasira, huku wengine wakiyarushia mawe magari yaliyokuwa yameegeshwa nje ya ukumbi huo.
Wafanyakazi katika ukumbi wa Mamba walilazimika kubadilisha mavazi yao ya kazi ili wasiweze kutambulika kiurahisi na mashabiki wa Ipupa, mpaka wakati ambao polisi waliingilia kati na kuidhibiti hali hiyo ya kutatanisha.
Bendi ya msanii huyo ililazimika kwenda jukwaani ili kuwatuliza mashabiki ambao kwa wakati huo walikuwa wanadai kurudishiwa pesa zao, wakitishia kumfungulia mashtaka Fally Ipupa pamoja na mmiliki wa klabu hiyo.


Siku moja kabla ya tukio hilo, msanii huyo alikuwa katika ukumbi mmoja jijini Nairobi katika tamasha ya Rhumba Night ambako pia alizua hali ya mshike mshike na isitoshe anadaiwa kuwapokonya baadhi ya wanahabari kanda zao.
Waandalizi wa tamasha hiyo walisita kutoa maoni yao kuhusu yaliyojiri usiku huo katika ukumbi wa Mamba mjini Mombasa.

Wednesday, July 20, 2011

Hii ni sehemu mojawapo muhimu ya jiji la Dar! Hebu angalia....

Mtaro ukiwa umefurika maji taka katika barabara ya Shaurimoyo eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam,ambapo ni hatari kwa magonjwa ya mlipuko pia wafanyabiashara wa eneo hilo wameendelea na shughuli zao bila kujali athali za kiafya zinazoweza kutokea.Picha na Michael Jamson