Tuesday, September 13, 2011


Nasi tukawa na maongezi yetu pia
Shukrani kwa wenyeji


Shukrani toka kwa mama mdogo wa bwana harusi mtarajiwa




Baada ya hapo tukahitimisha kwa msosi wa kukata na shoka









Tukawa busy na msosi wetu
Kama kawa

Huyu mama yangu mdogo
Baada ya hapo tukapiga picha wooote
Hapa nipo na wachumba, kushoto ndiyo mwenyewe na kulia ni binamu yangu Nadya







Mama yangu kushoto, Munira na mama yangu mdogo
Mama yangu kushoto, Munira na mama yangu mdogo
Hapa mama, mama yangu mdogo na dada yangu, Rehema

Dada yangu na wifi yake


Mimi, Munira na Uncle



Tuesday, August 23, 2011


Mtoto wa Gaddafi asema hajakamatwa, aapa atapambana hadi kieleweke!

Mtoto wa kiume wa kiongozi wa Libya, kanali Muammar Gaddafi, Seif Al Islam, amejitokeza hadharani katika hoteli moja mjini Tripoli na kukanusha madai kuwa amekamatwa.

Habari zinasema kuwa, Al Islam aliibuka katika hoteli hiyo jana asubuhi ambayo waandishi wa habari wa kigeni wamekuwa wakiishi mjini hapo na kuwaeleza waandishi hao, wananchi wa Libya na dunia kwa ujumla yupo salama na ataendeleza mapambano mpaka kieleweke.

Mwendesha mashtaka mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), Luis Moreno-Ocampo, na waasi wa Libya walisema juzi kuwa mtoto huyo wa Gaddafi wamemkamata.

Seif amesema utawala wa Gaddafi bado unaudhibiti mji mkuu Tripoli na kwamba baba yake yuko salama na katika hali nzuri mjini humo.

Al-islam ambaye alionekana kuwa mchangamfu na mwenye shauku kuu aliongeza waasi wameingia kwenye ''mtego'' mjini Tripoli na kwamba wanajeshi wanaomuunga mkono Kanali Gaddafi walikuwa ''wamevunja uti wa mgogo wa waasi hao''.


"Niko hapa kuuondoa uwongo uliotangazwa" alisema Saif Al-Islam mbele ya kikundi cha waandishi wa habari mjini Tripoli katika kitongoji cha Bab al- Azizyah ambapo ni makao ya baba yake.

“Mji mkuu Tripoli ungali uko chini ya udhibiti wa utawala wa baba yangu na kwamba Magharibi ilitumia teknolojia yake kuvuruga mifumo ya mawasiliano na kutuma jumbe kwa wananchi kwamba utawala wa Gaddafi umeanguka,” alisema Al- Islam.


Mtoto wa kiume wa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, Seif Al Islam akiwa na wafuasi wake pamoja na waandishi wa habari, akionyesha alama ya ushindi ya V baada ya kuibuka katika hoteli moja mjini Tripoli jana asubuhi. Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC), Luis Moreno-Ocampo, na waasi wa Libya walisema juzi kuwa mtoto huyo wa Gaddafi wamemkamata.

Sunday, August 21, 2011


Mambo matano ya kuiweka juu Chelsea

Mafanikio ya Chelsea yanategemea juhudi za wachezaji mmoja mmoja na timu yote kwa ujumla.
Chelsea ina wachezaji wazuri, lakini si kila mara wachezaji hao wamekuwa wakicheza kwa kiwango kikubwa. Katika soka hicho si kitu cha ajabu, kuna wakati mchezaji anaweza kuwika na kuna wakati anaweza kushuka kiwango na kuacha watu wakiwa midomo wazi.
Vilevile kuna baadhi ya wachezaji huwa ni muhimu katika klabu zao kuliko wengine, hiyo inategemea nafasi ya mchezaji, aina ya uchezaji na kocha anampanga mara ngapi. Chelsea nayo ina wachezaji muhimu na wengine wana umuhimu wa wastani.
Makala hii inawachambua wachezaji watano wa Chelsea ambao ni ngao ya kikosi, ambao wanaweza kuchangia kupatikana kwa ubingwa msimu huu.

5. Petr Cech
Timu zote hung'aa zinapokuwa na beki wa maana. Kama timu ina kipa mzuri, hiyo ni hatua ya kwanza kuelekea katika mafanikio. Chelsea ina bahati kwa kuwa ina kipa makini, Petr Cech. Cech amekuwa mkongwa katika kikosi cha Stamford Bridge. Ameidakia Chelsea mechi zaidi ya 300 na kuna dalili kwamba ataendelea kucheza katika klabu hiyo kwa miaka kadhaa.
Cech mwenye umri wa miaka 29 anadaiwa kuwa ndio kipa mzuri zaidi katika Ligi Kuu England kwa sasa. Mchezaji huyo yupo katika kiwango cha hali ya juu, anaweza kupigana na presha zote za Ligi Kuu England na michuano mingine ya kimataifa. Kama wachezaji wa ndani wakifanya vizuri huku Cech akiboresha kiwango chake mambo yatakuwa mazuri.


4. Winga
Hapa hatajwi mchezaji yeyote kwa kuwa nafasi ya winga ya Chelsea ni nzuri. Lakini winga wa Chelsea wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kusababisha usumbufu kutoka pembeni badala ya katikati kama walivyofanya mara kadhaa msimu uliopita.
Ikumbukwe kuwa hakuna timu inayoweza kutisha sana kama ikitegemea mipira ya kati pekee.

3. John Terry
Umri wa Terry unaweza kuwa umesonga kidogo, lakini nahodha huyo wa Chelsea anabaki kuwa mmoja wa mabeki wa kati wazuri duniani.
Chelsea inajivunia kuwa na beki huyo na amekuwa akiwaokoa katika hatari nyingi.
Mchezaji huyo ni mzuri kwa mipira ya juu na chini, ni wazi kuwa ataisaidia timu yake kufanya vizuri msimu huu.
Kama Terry akiumia au asipokuwepo uwanjani ni rahisi kuona Chelsea ikihangaika kufanya vizuri. Hiyo inaamisha kuwa uongozi wa Chelsea unatakiwa kuomba mchezaji huyo asishuke kiwango katika siku za karibuni la sivyo mambo yatakuwa magumu.

2. Frank Lampard
Watu wamekuwa wakizungumza mambo tofauti juu ya Frank Lampard, wengine wanasema ameanza kuishiwa, wengine wanasema baada ya muda mfupi ataondoka. Lakini bila kujali watu wanasema nini, ukweli ni kuwa Lampard ni mmoja kati ya wachezaji wazuri na hana dalili ya kustaafu karibuni.
Kweli, umri wake umesonga, lakini mchezaji huyo mwenye miaka 33 bado ana kiwango kikubwa. Huenda akapata shida kwenda sambamba na staili ya kocha mpya Andre Villas-Boas, lakini baada ya muda mfupi atasimama.
Tayari Lampard amejinoa vya kutosha katika mechi za kujiandaa na msimu na sasa anatakiwa kuendelea na kasi hiyo.
Lampard ni mchezaji mzuri na klabu yake inamtegemea kufanya mambo makubwa.

1. Didier Drogba/Fernando Torres
Chelsea inahitaji mabao ya kutosha.
Klabu hiyo ina washambuliaji wawili wazuri duniani lakini mmoja wao anatakiwa kuanza mara kwa mara.
Andre Villas-Boas amepanga vizuri maeneo mengine lakini linapokuja suala la washambuliaji anaonekana kuwa na wakati mgumu.
Didier Drogba na Fernando Torres wote ni wachezaji wa daraja la kwanza duniani lakini hakuna mchezaji kati yao, ambaye ameonyesha kiwango kwenye kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Watu wanaweza kusema umri wao umesonga lakini si kweli kwani Torres ana miaka 27. Kinachotokea hapo ni suala la kujiamini.
Drogba ni mchezaji mzuri lakini amekuwa akiwekwa nyuma ya Torres, na hiyo inamuondolea kujiamiani kwa kiasi fulani. Torres, ambaye alitua katika timu Januari bado hajafanya vizuri uwanjani.


Hitimisho
Kocha mpya anatakiwa kutafuta mbinu ya kuwapanga washambuliaji la sivyo hadithi yao itakuwa kama ya kocha wa zamani Carlo Ancelotti. Iwapo kocha akipata seti nzuri, kikosi kitafanya makubwa ziadi.

Vitimbi vya Mourinho vyamchefua Guardiola
Vitimbi vya kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho vimemchefua kocha wa Barcelona, Pep Guardiola.
Mourinho alikwenda kwenye benchi la ufundi la Barcelona na kuchoma kwa kidole chake kwenye jicho la kocha msaidizi wa timu hiyo wakati wa mechi kati ya timu hizo mbili, Jumatano iliyopita.
Katika pambano la Super Cup lililotawaliwa na ubabe, Real Madrid ililala 3-2 katika Uwanja wa Nou Camp.
Kwa matokeo hayo ikawa imefungwa jumla ya mabao 5-4 na Barcelona ikanyakua taji hilo. Timu hizo zilifungana 2-2 , Jumapili iliyopita kwenye mechi ya kwanza.
Beki wa Real Madrid, Marcelo alitolewa kwa kuonyeshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu mbaya kiungo mpya wa Barcelona, Cesc Fabregas.


Kitendo hicho kilisababisha zogo baina ya makocha wa timu hizo.
Mourinho alimfuata kocha msaidizi, Tito Vilanova na kumchoma jichoni kwa kidole na baadaye kumfanyia mzaha kama anambusu.
Guardiola alilalamika: "Kila mtu ameona kilichotokea. Kuna vitu havitakiwi kutokea katika mchezo wa soka."
"Kwa kweli tabia hizi hazipaswi kuachwa kuendelea."
Mourinho alijitetea kuwa hakufahamu nani aliyemchoma jichoni.