Vifaru na magari ya kijeshi yakipita mbele ya jukwaa kuu wakati wa mazoezi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru katika uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam, jana. Kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa kesho Desemba 9 uwanjani hapo.
Wasamaria wema wakijaribu kuwanasua abiria waliokuwa kwenye daladala aina ya Hiace, linalofanya safari kati ya Tabata Hai na Majumba Sita Ukonga, ambapo liliacha barabara na kugonga kituo cha Daladala cha Tabata Relini na kusababisha kifo cha mtu mmoja jijini Dar es Salaam leo.