
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, (Mahusiano na Uratibu) Stephen Wasira, amekiri kulala bungeni wakati kikao cha bunge kikiwa kinaendelea lakini, akalilaumu our sister paper Mwananchi, for taking a photo of him in such a circumstance.
Juni 22 mwaka huu katika toleo lake namba 04013, gazeti hili lilichapisha picha ya Wasira akiwa amefumba macho na kuinamisha kichwa begani wakati anakaimu nafasi ya Waziri Mkuu bungeni.
"Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Steven Wasira, akitafakari wakati wabunge wakichangia Hotuba ya Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2011/1012. Kutokana na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kutohudhuria kikao cha bunge juzi na jana (20 na 21 Juni), Wasira ndiye aliyekuwa akikaimu nafasi ya Kiongozi wa Shughuli za Serikali bungeni," ilieleza picha hiyo.
Juzi jioni Wasira wakati akifanya majumuisho ya Matumizi ya Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu alilishambulia gazeti hili kwa kumpiga picha hiyo, akisema linaandika habari za uchochezi.
Alithibitisha madai yake hayo kwa kutumia picha hiyo aliyopigwa akionekana amelala bungeni.
“Gazeti hili lina mlengo wa kigeni kila wakati linafanya mambo ya kichochezi, hawafai hawa,” alisema Wasira.
Wasira alikiri kuwa alikuwa amesinzia wakati Bunge likiwa linaendelea lakini, akasema kitendo cha gazeti hili kutoa picha yake akionekana amelala, ni uchochezi.
“Mheshimiwa Spika, mimi siku ile nilikuwa najisikia vibaya nikapitia hapo dispensary (zahanati ya Bunge) wakanipatia dawa ya mafua,”alijitetea Wasira ambaye ni mbunge wa Bunda akibainisha kuwa kwa kawaida, dawa aliyopewa ina tabia ya kusababisha usingizi.
Kwa mujibu wa Wasira Gazeti la Mwananchi lilitoa picha hiyo kwa lengo la kuchochea huku akitaja baadhi ya habari alizodai kuwa ziliwahi pia kutolewa na gazeti hili kwa lengo la uchochezi.
“Kwa mfano gazeti hili liliandika ‘Vita ya Lowassa, Serikali ya JK sasa wazi’ na nyingine ikaandika ‘Chadema yaibwaga CCM kuhusu posho,” alisema Wasira huku akinukuu vichwa vya habari hizo.
Wasira ametoa mtazamo wake huo dhidi ya gazeti hili, karibu wiki mbili tangu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali, Augustino Mrema kulisifu Mwananchi kuwa ni gazeti Makini, linalotoa habari za kweli na uhakika. Mrema pia aliwahi kupigwa picha na gazeti hili akiwa amelala bungeni.
Vile vile mashambulizi ya Wasira yamekuja wakati wabunge kadhaa wamekuwa wakitumia habari zilizoandikwa na gazeti hili nukuu habari za gazeti hili kujenga hoja zao bungeni, wakilieleza bunge kuwa kutokana na umakini wake, habari zinazoandikwa na Mwananchi ni za kuaminika.
Mmoja wa wabunge hao ni Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Susan Lyimo ambaye akitumia nukuu za gazeti hili aliliambia bunge kuwa Mfuko wa Rais wa Kujitegemea (PTF) umekuwa ukijihusisha na vitendo vya kitapeli.
“Mfuko huu umekuwa na tuhuma za kuwatapeli wananchi kwa kuwapa ahadi za wongo au zisizotimizwa kwa wakati. Mathalani Julai 15 mwaka jana, zaidi ya wanachama 200 wa mfuko huo wa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam walivamia ofisi ya makao makuu ya taasisi hyo yaliyopo Morocco Jijini Dar es Salaam wakilalamika kutapeliwa fedha zao za amana,” alilalamika.
Susan akionyesha kuwa taarifa hizo ni kwa mujibu wa Gazeti la Mwananchi la Julai 2010 pamoja na mtandao wa YouTube, alifafanua kuwa wanachama hao walikuwa wameambiwa watoe Sh18,000 kama kiingilio cha uanachama na amana ya Sh250,000 kwa ahadi ya kukopeshwa Sh1 milioni ndani ya kipindi cha wiki moja.
Mbaya zaidi alisema, wanachama hao waliongezewa vifungu vya masharti kwenye mikataba hiyo tofauti na awali hivyo kuwaweka katika wakati mgumu wa kupata mikopo waliyokusudia.
“Mheshimiwa Spika, wananchi wamefikia hatua ya kuufananisha mfuko huu wa rais na kampuni ya DEC ambayo ambayo inatuhumiwa kuendesha mchezo wa upatu kinyume cha sheria,” alisema Susan katika hutuba hiyo ya Kambi ya Upinzani wakati ambapo pia bajeti ya Mahusiano na Uratibu Ofisi ya Rais, ilikuwa imesomwa na Wasira.
Alisema PTF ilianzishwa kwa lengo l kuwawezesha wananchi wa kipato cha chini kwa kuwapamikopo na maarifa lakini malalamiko ya wananchi yanaashiria mfuko huo unaenda kinyume na kazi hiyo.
“Tumegundua kuwa mikopo inayotolewa na mfuko huu imekuwa na riba sawa na taasisi nyingine zinazofanya biashara ya kukopesha fedha,” alilalamika akifafanua:
“Sisi kambi ya upinzani tunahoji, je faida inayotengenezwa na mfuko huu inakwenda wapi? Mbona haionekani kwenye mapato ya serikali?”
Kibaya zaidi kwa PTF aliema
Kwa sababu hiyo, Susan alilitaka Bunge kujadili mwenendo na utendaji wa mfuk huo na kushauri njia bora ambayo itakuwa kwa maslahi yaliyokusudiwa.