Naomi awapiga jeki Red Cross
Mwanamitindo Naomi Campbell ametoa kitita cha pauni 94,000 (sh. 231 milioni) kwa ajili ya Shirika la Msalaba Mwekundu.
Campbell ametoa fedha hizo ili kusaidia watu walioathirika na kimbunga cha tsunami nchini Japan.
Naomi hivi karibuni aliandaa maonyesho ya mavazi huko Cannes, Ufaransa kwa ajili ya kuchangia fedha za kusaidia watu wa huko Japan.
"Mara nyingi tumekuwa tukiandaa maonyesho ya mavazi sehemu mbalimbali duniani ili kusaidia watu wenye matatizo mbalimbali."
Mastaa wa fani mbalimbali walichangia fedha ili kusaidia watu wa Japan, ambao pia waliathirika na kulipuka kwa mitambo ya nguvu za nyuklia.