
Sunday, October 2, 2011
Umri kikwazo cha Drogba Ulaya

Waafrika wanaokimbizana kwa utajiri Ulaya




Melissa Etheridge awakawaka

Lil Wayne ajivunia ukubwa

Jennifer Hudson kufungua gym

Lady Gaga akosa mvuto

Shakira apendelewa tuzo za Latin Grammy

Mourinho awafukuza kazi makocha Inter Milan




Friday, September 30, 2011
Kweli Mwananchi linaongoza!!
Tuesday, September 27, 2011
Hatimaye mdogo wetu aenda India kwa matibabu
Lazima kieleweke!
Igunga bado, hebu tuombe mambo yaende vizuri Inshaallah
Ajali haina kinga, IGP chupu chupu
Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Said Mwema (kulia) akifalijiwa na msamaria mwema baada ya kunusurika katika ajali ya gari iliyotokea juzi katika Barabara ya Kivukoni Front, mbele ya Ofisi za Takwimu na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Gari ya IGP iliyokuwa ikitokea Magogoni iligongana na gari ndogo.
Malori saba ya sukari yakamatwa Tarime
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Deusdedit Kato (kushoto), akiwa na maofisa wa jeshi hilo mbele ya magari yaliyokamatwa kwa madai ya kukutwa yamebeba sukari kupeleka kuuzwa nchini Kenya.
Polisi Mkoa wa Tarime/ Rorya wamekamata malori saba ya sukari yaliyobeba tani 93.70, kutokana na operesheni ya kupambana na magendo iliyoshamiri ya uvushaji sukari kwenda Kenya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tarime/Rorya, Deusdedit Kato, alisema walikamata mifuko 49 yenye ujazo wa kilo 50 kila mmoja nyumbani kwa mkazi wa Sirari. Alisema tani 2.45 zilitoka Tarime na tani 91.25 Musoma.
Kato alisema kwenye ukamataji walibaini mbinu ya kuhamisha sukari kutoka kwenye mifuko yake ya asili na kuwekwa mifuko mingine, ambayo ilikamatwa ikiwa tupu ya Kampuni ya Sukari Kilombero, huku sukari ikiwa imeondolewa.
Alisema sukari hiyo ilikuwa imejazwa upya kwenye mifuko ya South Nyanza Sugar ya Kenya na kwamba, shughuli hiyo hufanyika nchini na nje ya mpaka wa Tanzania, ili isafirishwe kwa urahisi kwenda Kenya.
Kato alisema maghala mengi yaliyopekuliwa hayakuwa na sukari, inasadikiwa yameficha bidhaa hiyo baada ya kutangazwa operesheni na kuongeza kuwa, imebainika sukari ya Tanzania huingizwa Kenya kwa ushirikiano wa wahalifu wengine kutoka Kenya.
“Kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola na taarifa za kiintelijensia, tumeendesha operesheni hii kwa kukagua maghala yote na kuwahoji wahusika. Pia, tumeongeza doria kwenye njia zote za panya na halali, tumekamata mifuko ya sukari mingine ni ya hapa Tarime na malori mengine yamekamatiwa Musoma wakidai kuwa walikuwa wanakuja kuuza Tarime," alisema
Monday, September 26, 2011
Wanawake kushiriki uchaguzi Saudia

Wanaume nchini Saudi Arabia kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi hiyo wameruhusiwa kushiriki kwenye uchaguzi.
Mfalme wa Saudi Arabia ametoa agizo akiwaruhusu wanawake kushiriki kama wagombea kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Baraza la Ushauri.
Sheria za Saudi Arabia zinawazuia wanawake wa nchi hiyo kushiriki kwenye shughuli zozote za kisiasa na pia kuwa na simu za mkononi na vilevile leseni za kuendeshea magari.
Ukiukwaji huo wa haki za wanawake huko Saudia ni mkubwa kwani wanawake wa nchi hiyo hawaruhusiwi hata kuingia kwenye maeneo mengi ya umma bila ya kuwa na mawalii au wasimamizi wao wa kiume.
UN yaanza kuijadili Palestina

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa jana limeanza kushauriana kuhusiana na ombi la Palestina kutaka uwanachama kamili wa umoja huo, ingawa kura kwa ajili ya ombi hilo haitarijiwi kufanyika mnamo majuma kadhaa yajayo.

Marekani imetishia kutumia kura yake ya turufu kupinga ombi hilo, ikisisitiza kuwa ni mazungumzo tu ya ana kwa ana kati ya Israel na Palestina ndiyo yatakayoweza kuzaliwa kwa taifa la wapalestina.
Pande nne zinazojihusisha na amani ya Mashariki ya kati, Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya, Marekani na Urusi zimekuwa katika juhudi za kutaka njia ya kuyafufua mazungumzo kati Israel na Palestina.
Bill Clinton amshambulia Netanyahu
Rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, amesema Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu, ndiye aliyesababisha kukwama mwenendo wa amani ya Mashariki ya Kati.

Katika mazungumzo yake ya kidiplomasia pembezoni mwa kikao cha 66 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Clinton amesisitiza kuwa, Netanyahu ndiye anayebeba dhima ya kukabiliwa na mkwamo mwenendo wa amani ya Mashariki ya Kati.
Madai hayo ya Bill Clinton anayatoa katika hali ambayo, daima Marekani imekuwa ikiuunga mkono utawala wa wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi wa Palestina.
Hayo yanajiri katika hali ambayo, Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina amewasilisha katika Umoja wa Mataifa ombi la Wapalestina la kutaka kutambuliwa nchi yao huru katika umoja huo, ambapo Marekani imetangaza wazi kwamba, itaupinga mpango huo na kwamba, itaupigia kura ya veto.
Prof Wangari Maathai afariki dunia

Mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel kutoka Kenya, Profesa Wangari Maathai (Pichani), amefariki dunia hospitalini mjini Nairobi alikokuwa akitibiwa saratani.
Profesa Maathai, aliaga dunia juzi usiku hospitalini hapo alikokuwa anapewa matibabu.

Habari zinasema, Maathai, aliyeshinda tuzo hiyo mwaka 2004, alikuwa muasisi wa Shirika la Mazingira nchini Kenya.
Profesa Karanja Njoroge ambaye ni Mkurugenzi wa Green Belt Movement, shirika ambalo Prof Maathai alilianzisha amethibitisha kifo hicho.
Katika taarifa kwa vyombo vya habari Prof Njoroge alisema wakati wa kifo chake Wangari alikuwa na wanafamilia na marafiki.
Alisema Prof Maathai ambaye alikuwa na umri wa miaka 71, ameacha watoto watatu, wawili wakiume na mmoja wa kike.
Waasi wagundua kaburi lenye maiti 1,270 Tripoli

Ofisa wa Baraza la Mpito nchini Libya (Kulia), akiwaonyesha wapigapicha baki la sare ya gerezani ambayo imepatikana katika kaburi la pamoja la miili ya wafungwa zaidi ya 1,270 iliyogunduliwa na baraza hilo mjini Tripoli juzi. Mabaki hayo yanadhaniwa kuwa ya wafungwa waliouawa na maofisa wa usalama mwaka 1996 katika gereza la Abu Salim nchini humo.
Baraza la Mpito nchini Libya limesema kuwa, wameligundua kaburi la pamoja mjini Tripoli ambalo lina maiti 1,270.
Mabaki hayo yanadhaniwa kuwa ya wafungwa waliouawa na maofisa wa usalama mwaka wa 1996 katika gereza la Abu Salim.
Uasi dhidi ya Kanali Muammar Gaddafi ulianza kama maandamano kutaka wakili aliyewakilisha familia za wafungwa wa Abu Salim aachiliwe huru.
Uchimbuaji wa kaburi hilo la pamoja unatarajiwa kuanza hivi karibuni.


