Friday, April 13, 2012

Ali Kiba ahojiwa polisi kwa kumpa lifti Lulu

Ali Kiba

Msanii wa muziki wa Bongo Flava, Ali Kiba, anadaiwa kuhojiwa na polisi kwa maelezo ndiye aliyempa Elizabeth Michael ëLuluí msaada wa usafiri (lifti) baada ya kutoka kwa Steven Kanumba.
Lulu ndiye anayetuhumiwa kuhusika na kifo cha Kanumba kilichotokea usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita.
Kachelo aliyemhoji Lulu Jumatatu wiki hii, amedai kuwa msanii huyo alihojiwa katika kituo cha Polisi cha Oysterbay kutokana na kutajwa na mtuhumiwa kuwa ndiye aliyempatia lifti baada ya kutoka kwa Kanumba.
Mwanaspoti lilimtafuta Ali Kiba ili azungumzie taarifa hizo, alipopatikana kwa njia ya simu, msanii huyo alisema: ìSamahani kaka siwezi kuzungumzia chochote kuhusu mambo hayo.î Kisha akakata simu.
Lulu alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jumatano wiki hii na kutotakiwa kujibu chochote kwa vile mahakama hiyo haina uwezo wa kisheria wa kusikiliza kesi za mauaji.
Lulu alitoa maelezo yake polisi Jumatatu ikiwa ni saa 65 tangu kutokea kwa kifo cha Kanumba., ambapo alizungumza na kachero wa Makao Makuu ya Polisi ambaye pia ana taaluma ya saikolojia.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Jeshi la Polisi zinaonyesha kuwa kachero huyo (jina tunalo) aliyetoka makao makuu alifanikiwa kufanya mahojiano na binti huyo ambaye awali aligoma.
Imeelezwa kuwa, alitumia takribani sasa tatu kumlainisha Lulu azungumze.
Katika mahojiano , kachero huyo ambaye alitoka katika Kitengo cha Upelelezi wa Makosa ya Jinai alisema tayari amemhoji mtuhumiwa namba moja Lulu pamoja na msanii huyo maarufu wa muziki wa kizazi kipya kufuatia kifo cha Kanumba, aliyefariki usiku wa kuamkia Jumamosi.
Akimnukuu Lulu katika mazungumzo yake, kachero huyo alisema Lulu aliitwa na marehemu Kanumba ili waweze kutoka (out) kwenda kwenye bendi ya Mashujaa ambayo ilikuwa inapiga kwenye kiwanja chao cha nyumbani, Vingunguti.
Lulu

Mtuhumiwa alionekana kutokuwa tayari, lakini marehemu ëakamlazimishaí.
Kachero huyo alisema: "Lulu anadai alifika nyumbani kwa marehemu saa tano usiku, lakini akiwa ameweka msimamo wa kutokwenda sehemu yoyote usiku ule, lakini Kanumba alikuwa akilazimisha ndipo yakatokea mabishano na marehemu akafunga mlango kwa funguo.
"Hata hivyo, baada ya ugomvi wa kama nusu saa hivi, Lulu alifanikiwa kuondoka chumbani humo na alifungua mlango kwa taharuki na kuondoka bila kujua kilichotokea nyuma, huku akimweleza ndugu wa marehemu kwamba Kanumba ameanguka."
Mpashaji habari wetu huyo alisema, kumekuwa na jumbe fupi za maneno kutoka kwa wanasiasa ambazo zimekuwa zinaingia kwenye simu ya kiganjani ya Lulu, zikiahidi kumsaidia.
Alionya kuwa kama wanasiasa wataanza kuingilia uchunguzi wa Polisi katika kesi hiyo ambayo imevuta hisia za watu wengi, wanaweza kuharibu mambo. Lakini yeye mwenyewe akionyesha kwamba yuko imara na anafahamu anachokifanya.
Kuhusu msanii wa muziki wa kizazi kipya, Ali Kiba, kachero huyo alisema kwamba alihojiwa kutokana na kutajwa na mtuhumiwa kama mtu aliyempatia msaada wa usafiri (lifti) baada ya kutoka kwa Kanumba.
Kachero huyo alisema kutokana na taarifa ambazo wanaendelea kuzipata, kuna uwezekano watu wengi zaidi wakahojiwa ili kujiridhisha kabla ya ëwatuhumiwaí kuanza kupandishwa kizimbani baada ya upelelezi kukamilika.

MCT yawaonya wanahabari kuhusu ‘Lulu’


Baraza la Habari Tanzania (MCT), limewaasa waandishi wa habari kuzingatia maadili ya kazi yao hasa wakati huu wa kuripoti kesi inayomhusu Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili wa MCT, Jaji Mstaafu Thomas Mihayo alisema kuwa wadau wa tasnia ya habari wamekuwa wakimuhukumu moja kwa moja Lulu kuwa ndiye aliyemuua Steven Kanumba.

“Kwa mjibu wa sheria na maadili ya uandishi wa habari mtu yeyote anayekamatwa kwa tuhuma yoyote ile ni mtuhumiwa mpaka atiwe hatiani na mahakama,” alisema Jaji Mihayo na kuongea:

“MCT inasikitishwa na baadhi ya vyombo vya habari kwa ukiukwaji wa maadili uliojitokeza wakati vikiripoti kuhusu kifo cha Kanumba, vimemuhukumu Lulu kuwa ameua kinyume na maadili ya kazi yao.”

Jaji Mihayo alisema kuwa MCT kwa nyakati tofauti imekuwa ikitoa matamko yanayowakumbusha wanahabari kujiepusha na uandishi wa habari au vichwa vya habari vinavyohukumu.

“MCT inatambua fika kesi zilizoko mahakamani ni kivutio kwa umma kutaka kujua kinachopendelea ili kuona haki ikitendeka na pia wanahabari wana haki ya kujua na kuripoti yanayojiri huko na katika vyombo vingine vya sharia,” alisema Jaji Mihayo na kuongeza:

“Wanahabari ni lazima watambue kuwa kuna taratibu na makubalianao ya kijamii juu ya namna taarifa zinavyopaswa kuripotiwa ili kutowadhuru watu wengine.”



Naye Katibu Mkuu wa (MCT), Kajubi Mukajanga alisema kuwa mwandishi wa habari ana uwezo wa kuifanya jamii ikaamini na kumfikiria Lulu moja kwa moja kuwa ndiye aliyemuua Kanumba jambo ambalo si kweli mpaka lithibitishwe mahakamani.

Kuhusu taarifa ambazo zimekuwa zikienezwa na mitandao ya kijamii kuhusu kifo cha Kanumba kuwa zimesabishwa na Lulu alisema Mukajanga alisema kuwa MCT hawahusiki na mitandao hiyo.

Mukajanga alisema atafuatilia kujua nini kilisababiaha kuwepo kwa usiri kwa polisi kutotoa taarifa ya wapi Lulu alitakiwa kufikishwa mahakamani ili waandishi wa habari wapate nafasi ya kufanya kazi yao.


Tuesday, April 10, 2012

Hatimaye Steven Kanumba apumzishwa katika nyumba yake ya milele

















Mayowe yalianza, vilio kila kona baada ya jeneza lenye mwili wa marehemu kuingia katika Viwanja vya Leaders Club




Waombolezaji walishindwa kuzuia hisia zao






















Wema, Aut nao walikuwapo kutoa heshima zao za mwisho kwa marehemu.








Irene Uwoya akipatiwa matibabu baada ya kuzimia


Ukawa ni mwendo wa watu kuzimia tu











Hapa makaburini kuna umati mkubwa wa watu ambao haujapata kutokea. Jua ni kali sana. Hata hivyo, shughuli ya mazishi inaonekana kuendelea. Kuna waliokaa vivulini. Kuna waliopanda juu ya miti. Kuna waliopanda ukutani. Kulikuwa hakuna hata pa kupitia





Hapa makaburini hakuna aliye na wakati wa kuokota kandambili yake iliyokatika au kuvuka miguuni, nyingi zimelowana matope. Ajabu ya tope hili, sijui limetoka wapi wakati kuna jua kali linalokausha vichwa vya watu.


Hatimaye mdogo wetu akalazwa katika nyumba yake ya milele, sasa ndio tunaamini kuwa hatutomwona tena mpendwa wetu Steven Kanumba, ulale pema peponi... Amin